A PHP Error was encountered

Severity: Notice

Message: Only variable references should be returned by reference

Filename: core/Common.php

Line Number: 272

Donda | Blog
Fun!

Life Style

DONDAWivu kitu kibaya mwanaadamu kua nacho,
Wivu hukukosesha haya ukakufanya utoe macho,
Wivu hukupa ari ya kufanya maovu bila kicho,
Mwenye wivu hadiriki kufurahia alichonacho.


Wivu hukubadili akili alo mzuri ukamponda,
Wivu sawia na kidonda ukiufwata utakonda,
Wivu ni kujitia dhiki sasa vipi utawanda?
Mwenye wivu hukosa nguvu akashindwa hata kwenda.

Wivu ni sumu iliyoharibu watu duniani,
Wivu umefanya ndugu wakawa hawapatani,
Wivu hufanya mtu marafiki akawafitini,
Mwenye wivu akiingia watu hukosa amani.

Wivu hukufanya ukaharibia mtu jina,
Wivu hukupa nguvu ya uongo ukanena,
Wivu hukuhadaa ukajiona wewe ndio wina,
Mwenye wivu na hasidi tofauti hawana.

Wivu umegeuza watu wakawa hayawani,
Wivu umefanya watu kutiana mikononi,
Wivu asili kubwa ni kumshiriki shetwani,
Mwenye wivu huharibu mema kama moto ulavo kuni.

Wivu kuutambua rahisi wallahi,
Wivu kuna wakati huonekana kwenye wajihi,
Wivu kuujua zaidi ni mtu kukuekea inhi,
Mwenye wivu ukimuona sema Hasbiyallahi.

photo credit: Tambako the Jaguar via photopin cc

Comments

There are no comments

Post a comment