A PHP Error was encountered

Severity: Notice

Message: Only variable references should be returned by reference

Filename: core/Common.php

Line Number: 272

HAKUTAKA KUWA KIKOJOZI | Blog
Fun!

Life Style

Kuna watoto wengi ulimwenguni wana ‘tabia’ ya kukojoa kitandani wanapokua wamelala. Maarufu watoto hawa huitwa ‘vikojozi’. Ushawahi kujiuliza iwapo kuna mtoto yeyote anayetaka kuwa kikojozi? Je, unadhani mtoto hufurahia kila usiku kukatiza usingizi wake anapojisara  kwa harufu za mkojo? Mimi naamini  kuwa kikojozi ni maradhi kama maradhi mengine na mtoto anahitaji kupewa heshima na kutazamwa kama anavyotazamwa mtoto wa kawaida.

Mimi binafsi, nilikua kikojozi utotoni mwangu na hadi hii leo namshukuru mamangu kwa jinsi alivyonilea na kunitazama. Waliojifanya wajua kulea, walisema mamangu anitendekeza. Leo nawaambia, “Ndio alinitendekeza kwasababu ‘Uchungu wa mwana aujuwae ni mzazi.” Alijua fika sikutaka kukojoa kitandani na ili kupoa nilihitaji mapenzi ya mama mlezi na baba mpenzi (Mungu amrahamu).

Mamangu alihakikisha kuwa inapofika magharibi napunguza idadi ya maji ninayokunywa. Kabla ya kulala atahakikisha nimekwenda msalani kukojoa, kisha ndio aniruhusu nilale. Nyakati za usiku nilikua na usingizi ‘nusu nusu’. Yani kila baada ya masaa fulani naamshwa kwenda chooni. Hilo liliniharibia usingizi wangu pamoja na wa yule aliyekuwa akiniamsha, mamangu. Kitanda nacho nilitandikiwa mpira ndio pale nitakapokojoa nisitoteshe godoro.

Babangu naye (Mungu amrehemu) alikua na bidii ya kunitafutia matibabu. Nilikua na safari za nenda rudi kwa tabibu Khitamy (Mungu amrehemu). Dawa zake zilinisaidia japo kwa muda.

Nilikua kikojozi mpaka nilipomaliza darasa la nane. Wadhani kuna mtoto anayetaka kukojoa maksudi hadi umri huo?

Kwa maoni yangu, ujinga na ukosefu wa wapenzi ndio unaomfanya mzazi kumdhalilisha mwanawe anapokua kikojozi. Utapata mama/baba humpaka mtoto mashizi (vumbi la makaa) ya uso, akamvalisha nguo alizozikojolea, na kuita watoto wote wa mtaani kuja kumkejeli na kumuimbia, ‘Kindumbwendumbwe Chaaria. Kikojozi, kakojoa, na nguo zake kazitia mkojo.’ Isitoshe mtoto huyo licha ya umri mdogo, atalazimishwa kufua mpaka mabedshiti aloyakojolea. Huku ni kumfanya mnyonge mtoto wako na kumtia uoga mbele yako. WALLAHY hakusaidii lolote kumdhalilisha.

 

photo credit: Internet Archive Book Images via photopin (creative commons licence)

Comments

There are no comments

Post a comment