Current Affairs
IDARA ya Uchunguzi wa Jinai (CID) imewataka wamiliki wa kampuni
zinazodaiwa kujipatia ardhi kwa njia isiyo halali Lamu kuandikisha taarifa, huku
uchunguzi kuhusu ardhi katika kaunti hiyo ukishika kasi.
Mkuu wa idara hiyo Bw Ndegwa Muhoro alitangaza kwamba uchunguzi
utafanywa kwa pamoja na maafisa wa CID na wale wa Tume ya Maadili na
Vita Dhidi ya Ufisadi (EACC).
WAHUDUMU wa matatu wamepata matumaini baada ya Kamati ya Bunge
Kuhusu Usalama kupendekeza sheria kali za trafiki zilizoanza kutekelezwa na
serikali zifutiliwe mbali.Kamati hiyo ilisema sheria hizo zinakiuka katiba na ikapendekeza zibatilishwe.
MKUTANO ulioandaliwa na Waziri wa Ardhi Charity Ngilu kujadili masuala ya
ardhi katika Kaunti ya Kwale Jumatatu alasiri ulitibuka baada ya kuvamiwa na
nyuki. Nyuki hao walivamia afisi za ardhi muda mfupi tu baada ya mkutano huo
kuanza. Ziara yake afisini humo ililenga kuangalia shughuli za kupanga upya afisi hiyo aliyokuwa ameagiza ifungwe kwa siku 10.
SERIKALI imependekeza kanuni mpya ambazo zitawazuia waendeshaji wa
bodaboda kuhudumu katikati mwa miji yote kote nchini. Hatua hii huenda ikaathiri pakubwa biashara ya wahudumu hawa ambao wamekuwa mashuhuri katika miji mingi.

There are no comments