A PHP Error was encountered

Severity: Notice

Message: Only variable references should be returned by reference

Filename: core/Common.php

Line Number: 272

EBOLA VS HAJJ | Blog
Fun!

Insights

Huku mamilioni ya waislamu kote ulimwenguni wakijitayarisha kwa ibadah ya Hajj au Umrah, ndugu waislamu kutoka mataifa ya Sierra Leone, Guinea na Liberia watafungiwa nje kufuatia janga la Ebola katika mataifa hayo. Waziri wa Afya nchini Saudia Dkt. Khalid Marghalani  amesema kwamba waislamu kutoka mataifa hayo 3 ya Afrika Magharibi watanyimwa Visa za kusafiri kwa ajili ya Hajj kufuatia tishio la maambukizi ya virusi hatari vya Ebola.

 
Kwa mujibu wa jarida la International Business Times, kuna takriban waislamu millioni 13.5 wanaoishi Sierra Leone, Guinea na Liberia, huku Guinea ikiwa na idadi kubwa zaidi ya waislamu milioni 9.7. Hajj ni mojapo ya nguzo 5 za Uislamu, na kisheria inastahili Muislamu kuzuru mji mtakatifu wa Makkah (Mecca) angalau mara moja maishani mwake iwapo ana uwezo.

 
Na huku ugonjwa hatari wa Ebola ukiwa bado ni tishio kote duniani, Imam Mohammed Turay ambaye ni mwenyekiti wa baraza la kitaifa la maimamu nchini Liberia amewaonya waislamu dhidi ya kuosha maiti katika mataifa yanayokumbwa na janga la Ebola. Imam Turay amesisitiza kuwa Quran tukufu inakataza dhidi ya kugusa miili ya watu ambao huenda wamefariki kutokana na maradhi hatari.

 
Lakini mpaka sasa Ummah wa Waislamu katika mataifa hayo 3 ya Afrika Magharibi hayajapokea msaada wowote wa kifedha au kimatibabu kutoka kwa mataifa ya Kiislamu. Aghalabu, lazima ndugu waislamu kutoka mataifa yanayojiweza kuwasaidia ndugu hao wakati huu wa msiba wa Ebola, kwani mpaka sasa China ndio taifa la pekee ambalo limetuma misaada na madaktari huko Sierra Leone, Guinea na Liberia.


 

Yako wapi mataifa stawi kama Bahrain, Qatar, Saudia na Dubai? Ummah wa Waislamu kutoka Afrika Magharibi unawahitaji wakati huu wa shida.

 

photo credit: *Muhammad* via photopin cc

Comments

There are no comments

Post a comment