A PHP Error was encountered

Severity: Notice

Message: Only variable references should be returned by reference

Filename: core/Common.php

Line Number: 272

HABARI KWA UFUPI [dublicated-8] | Blog
Fun!

Current Affairs

Mwanafunzi mmoja afariki na wengine sita kuteketea baada ya moto kuteketeza bweni moja la shule ya Upili ya Tala iliopo Matungulu. Inadaiwa huenda moto huwa ulianzishwa kimakusudi na wanafunzi.

Moto mkubwa wateketeza mali ya thamani kubwa katika duka moja la kuuza nguo na magodoro mtaa wa Bomani mjini Malindi kaunti ya Kilifi. Wakaazi wamekashifu idara ya zima moto kwa kufika kuchelewa katika eneo la tukio. Kufikia sasa chanzo cha moto hakijabainika.

Watu wawili wauawa na wengine wawili wanauguza majeraha baada ya jamaa waliojihami kuvamia baa moja mtaani Majengo mjini Mombasa usiku wa kuamkia Jumatano.

Watu 80 wakamatwa na kushtakiwa papo hapo kwa kupuuza vivuko vya barabarani na badala yake kuvuka barabara kiholela katika maeneo ya Pangani na Uwanja wa Kitaifa Nyayo. Wapita njia hao walikamatwa na maafisa wa trafiki na kushtakiwa na mahakama ya muda iliokuwa kando ya barabara.

Jamaa mmoja afumaniwa akila uroda na mbuzi mtaani Mkanyageni mjini Mombasa na kupewa kichapo cha mbwa aliyekojoa msikitini.

Wakimbizi 13 wenye asili ya Uhabeshi (Ethiopia) watiwa mbaroni katika kaunti ya Kirinyaga. Mkenya mmoja pia akamatwa kwa kuhusika na biashara ya kuwasafirisha.

Shirika la safari za ndege la Marekani la Federal Aviation limesema kuwa anga ya Kenya ni hatari kwa safari za ndege na kushauri ndege za Marekani kutofika katika nyanja za ndege za Kenya. Tahadhari hii itakuwa pigo kubwa kwa taifa la Kenya.

 

Comments

There are no comments

Post a comment