Life Style
Maajabu haya!!!
Dunia ina vituko vya kila aina, ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni!
Huzuni au kufiliwa ni pigo kubwa sana, hususan iwapo yule aliyefariki ni rafiki azizi au mmoja wa watu wa familia yako kama wazazi, mumeo/mkeo au wanao wapendwa. Sisi waislamu Alhamdulillahi, imani na dini yetu ndio muongozo wetu. Ndio maana tukiondokewa na mtu twahuzunika na kumuombea dua tukijuwa ya kwamba njia ni hiyo hiyo na wala hakuna uhodari hapo (wa kukimbia kifo.)
Maombolezi hutegemea roho ya mtu, kuna wale wanaolia huku wakipiga mayowe na hata kujigonga ukutani na kujiumiza, kuna wale wanaojikaza na kulia moyoni, wengine husikitika pekee na wachache wenye roho ngumu huwa wanaangalia tu. Yote hayo ni mambo ya kawaida ela wengine wanavuka mipaka na kukufuru. Utasikia mtu alia huku yuwasema "Mume wangu/ mwanangu/ babangu ankufa sasa nani atatuangalia?!" Amesahau ya kuwa mwenye kumuangalia ni Mungu, na hao wengine ni sababu tu.
Sasa vituko viko hapa! Kuna jamii hii moja inaitwa 'Dani' ilioko sehemu ya Papua Magharibi nchini New Guinea. Jamii hii ina njia ya kipekee na ya kushangaza ya kuonyesha huzuni yao pale wanapofiliwa. Ndio nikasema hapo awali 'Dini ni muhimu jamani' tusiishi kama hayawani. Jamii hii inapofiliwa na mmoja wao basi watu wao (hususan wanawake) walio na uhusinao wa karibu na aliyefariki hujikata kidole kimoja kila wanapofiliwa.
Jamii hii inaamini mmoja wao anapofariki, basi mizimu yake husalia duniani. Kwa hivyo, ukataji wa kidole ni njia ya kuifukuza mizmu hii. Vilevile, jamii hii hujikata vidole kama ishara ya kuonesha masikitiko kwa kuondokewa na mpenzi wao. Kwa kawaida wanaanza na kidole kirefu, isipokuwa mzazi akifiliwa na mwanaye mchanga anaanza kukata kidole kifupi. Kando na kujikata vidole, wanawake hao hujisara nyuso zao kwa kutumia mashizi na udongo.

Mtu anapokufa basi hutumia kifaa kikali kukata kidole karibu na kaburi. Kwanza hukifunga kidole hicho kwa kukaza kifaa maalumu (au hata uzi) na baadae kusubiri kwa muda wa nusu saa. Alafu kisu, jiwe kali au hata kijishoka kidogo hutumiwa kukata kipande cha juu cha kidole. Kidole kinachosalia hufungwa kwa majani hadi kipoe. Kile kipande cha juu cha kidole kilichokatwa, huwekwa juu ya kaburi kwa masiku mpaka kinyauke, halafu kinachomwa mpaka kuwa majivu na kurushwa juu ya kaburi. Basi hapo huwa mizimu ya waliokufa hayawafikii majumbani mwao, naye aliyekufa huwa radhi pale alipolala.

Kifaa kinachotumika kufunga kidole kabla ya kukikata)
Mila hii potofu sasa imepigwa marufuku nchini humo japo kuna wanawake wengi wanaoishi bila ya vidole.
Tumshukuruni Allah (Subhaanahu Wataala) kwa neema hii ya akili, hekima na dini yetu tukufu. Tusemeni Alhamdulillah.
(Photo credits عجاءب وغراءب and ripleys.com)

There are no comments