Insights
2. KUFUNGA MWEZI WA RAMADHAANI
Baada ya kuzungumzia nguzo ya swala sasa sharti la pili linalofuata ni swaum katika mwezi mtukufu wa Ramadhaan. Ni wajib kwa kila muislam kufunga siku zote za Ramadhaan ila patakapo tokea udhuru wa kisheria. Kwa mfano ugonjwa, safari au hedhi na nifasi kwa mwanamke. Hapa ameruhusiwa kutofunga lakini baadae anatakiwa kuzilipa zile siku alizoziwacha kwa minaajili kukamilisha funga yake.
Wengi miongoni mwa wanawake hawatambui kuwa damu ya istihadha (ugonjwa) haimzuii mwanamke kuwacha kufunga. Wengine huchelewesha kujitwaharisha kutokana na hedhi au nifasi na kupitiliza muda mrefu bila ya kufahamu ya kuwa inawalazimu kujitwaharisha na kuanza kuswali na kufunga. Hapa ndipo panapokuja wajibu wetu wa kuisoma dini kiundani zaidi na kufahamu fiqhi ya ibada. Kwa hivyo ni wajibu wetu kuufunga mwezi wa Ramadhaan madamu hatuna nyudhuru za kisheria za kutufanya kutofunga.
Jambo la mwisho tufahamu ya kuwa Allah ni mjuzi wa yaliyomo ndani ya nafsi zetu, na kwamba tutakapo wacha kufunga na kudanganya binadamu wenzetu kuwa hatuko wasafi (twahara) huwa tunajidanganya wenyewe na Allah atatulipa kwa kila tulifanyalo.
3. KUHIFADHI UTUPU WAKE
Tukizungumzia suala la kujihifadhi utupu, kwanza tunazungumzia kujistiri mwili kwa mavazi ambayo tumeamrishwa tujihifadhi kwayo. Wanazuoni wameyafafanua mavazi yenyewe kuwa na masharti sita, nayo ni:
i. Yahifadhi mwili mzima.
ii. Yasibane.
iii. Yasionyeshe vilivyomo ndani.
iv. Yasiwe na manukato makali au kunukia sana.
v. Yasiwe na mapambo.
vi. Yasifanane na mavazi ya kikafiri.
Hayo ndio masharti ya mavazi anayotakiwa kuvaa mwanamke wa kiislam.
Pili tunazungumzia mwanamke kujihifadhi utupu wake kwa kutofanya uzinifu kwani uzinifu ni uchafu na ni mwenendo mbaya kama anavyotuambia Allah ndani ya Qur'an: “Wala msikaribie uzinifu. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya.” [Al-Israa 17 : 32].
Faahamu ya kuwa miongoni mwa sifa za waumini ni wale wanaojihifadhi na kujistiri miili yao kutokana na yale aliyowaharamishia Allah kama anavyotuambia Allah (Subhanahu Wata‘ala): “Na ambao wanazilinda tupu zao. Isipo kuwa kwa wake zao au kwa iliyo wamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa.” [Al-Muuminun 23 : 5-6].
.Jambo la mwisho kuhusu mavazi tambua ya kuwa vazi bora ni ucha Mungu. Kama ambavyo Allah (Subhanahu Wata‘ala) ameliita ndani ya Quran: “Enyi wanaadamu! Tumekuteremshieni nguo za kuficha tupu zenu, na nguo za pambo. Na nguo za ucha Mungu ndio bora. Hayo ni katika ishara za Mwenyezi Mungu mpate kukumbuka.” [Al-Araf 7 : 26]
4. KUMTII MUMEWE
Ewe dada wa kiislam uliyeolewa tambua ya kuwa Allah (Subhanahu Wata‘ala) amekuamrisha kumtii mumeo katika mambo ya kheri kama alivyokuamrisha ibada nyingine. Allah (Subhanahu Wata‘ala) anatuambia: “Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi ... ” [An-Nisaa 4 : 59].
Miongoni mwa wenye madaraka ni waume baada kukabidhiwa dhamana na wazazi wetu. Amesema mtume (Swalla Allahu Alayhi Wasallam): “Laiti ningekua naamrisha mtu kumsujudia mwenzake basi ningelimuamrisha mwanamke kumsujudia mumewe.” Tirmidhiy. Hadithi hii inaonyesha wazi nafasi aliyonayo mume kwa mkewe.
Pamoja na kuwa kuna mipaka katika maamrisho yake juu yako, lakini inakubidi kujitahidi kumtii ili uipate pepo kupitia yeye. Kwani amesema mtume (Swalla Allahu Alayhi Wasallam) katika hadithi: “Mwanamke yeyote aliyekufa hali ya kuwa mumewe yupo radhi nae, ataingia Peponi.” Tirmidhiy. Hadithi hii inaonyesha ya kuwa miongoni mwa mambo yanayompa utukufu na nafasi njema mwanamke aliyeolewa ni twa‘a kwa mumewe. Bila shaka mumewe hawezi kuwa radhi naye kama hatakuwa na utiifu kwake.
Hivyo tujitahidini kina mama katika suala hili kwani wengi wetu hatulitekelezi ima kwa kutojua au kutokana na kibri. Hali ambayo hupelekea kuharibika kwa ndoa nyingi bila ya wenyewe kufahamu hilo.
HITIMISHO
Fanya hima ewe mwanamke wa kiislam katika kuyatekeleza masharti haya manne ili uingie katika pepo ya Allah (Subhanahu Wata‘ala) kupitia mlango unaoupenda na ni kheri ilioje hii kwenu wanawake.
Bila shaka kina baba wanawaonea wivu kwani wao wamepewa masharti mengi zaidi kuliko yenu kama alivyoelezea Allah katika Suratul Muuminun na nyinginezo ndani ya Quran. Napenda kumalizia kwa Aya ya Allah isemayo: “... Na katika hayo washindanie wenye kushindana.” [Al-Mutwaffifiin 83 : 26].
Na Allah ni mjuzi zaidi.
(Photo credits theidealmuslimah.com)

There are no comments