A PHP Error was encountered

Severity: Notice

Message: Only variable references should be returned by reference

Filename: core/Common.php

Line Number: 272

MASHARTI MANNE YA KUMUINGIZA MWANAMKE PEPONI - Sehemu ya 1 | Blog
Fun!

Insights

Namshukuru Allah (Subhanahu Wata‘ala) kwa kunipa siha na nafasi ya kuandika mada hii. Swala na salamu zimuendee mtume wetu Muhammad (Swalla Allahu Alayhi Wasallam) aliyekuja na dini iliyompandisha mwanamke daraja na cheo kiasi cha kumrahisishia njia za kuingia peponi kwa kupewa masharti manne pekee. Masharti nitakayofafanua katika makala haya kwa Tawfiq ya Allah (Subhanahu Wata‘ala).

Katika hadithi iliyopokelewa na Imam Ahmad, amesema Mtume (Swalla Allahu Alayhi Wasallam): “Atakaposwali mwanamke swala zake tano na akafunga mwezi wake na akajihifadhi utupu wake na akamtii mumewe ataambiwa siku ya Qiyama ingia Peponi kupitia mlango unaoupenda.”

Sasa tutaanza uchambuzi wa sharti moja moja ili tuone nini kimekusudiwa.

1.   SWALA TANO

Ewe dada yangu muislamu tambua ya kwamba swala tano za faradhi ni wajibu kwako na ni miongoni mwa nguzo tano zinazojenga dini yako. Kuwacha nguzo hii ni kubomoa dini yako swala ndio nguzo thabiti Zaidi baada ya shahada. Vilevile, swala ndio tofauti iliyopo baina ya uislamu na ukafiri. Swala pia ndio usia wa mwisho aliyousisitiza sana mtume (Swalla Allahu Alayhi Wasallam) karibu na kufa kwake kwa kusema “Swala swala na wale iliyoimiliki mikono yenu” (yani watu wenu wa karibu).

Ewe dada wa kiislamu tambua ya kuwa Allah (Subhanahu Wata‘ala) amekurehemu kwa kukupunguzia ibada hii ya swala pale unapopatwa na ada zako ( hedhi na nifasi ) na wala hakukuamrisha kuzilipa. Hii ni kwa sababu ya huruma ya Allah (Subhanahu Wata‘ala) aliyonayo mbele yako. Sasa kama ni muumini wa kweli uliyezoea swala, basi baada ya kumaliza ada yako lazima uwe mchangamfu katika swala na sio kuwa mvivu kwani Allah (Subhanahu Wata‘ala) anatuambia ndani ya Quran tukufu: “Na tafuteni msaada kwa kusubiri na kwa kusali; na kwa hakika jambo hilo ni gumu isipokuwa kwa wanyenyekevu.” [Al-Baqara 2 : 45].

Pia kama utashikamana na swala basi hukuepusha na maovu, kama anavyotueleza Allah (Subhanahu Wata‘ala): “... Hakika Sala inazuilia mambo machafu na maovu ... ” [Al-Ankabut 29 : 45].

Vilevile, swala kama yalivyo mema mengine, hufuta maovu yako kama anavyotuelezea Allah (Subhanahu Wata‘ala): “Na shika swala katika ncha mbili za mchana na nyakati za usiku zilizo karibu na mchana. Hakika mema huondoa maovu. Huu ni ukumbusho kwa wanao kumbuka.” [Hud 11:114].

Kwahivyo, ewe mwanamke wa kiislamu shikamana na swala kwani itakufaa hapa duniani mpaka kesho akherah. Kwani swala yako ndio itakayo hesabiwa mwanzo, na itakapotengenea swala yako basi ni bishara njema kwako na itakapoharibika utakua ni miongoni mwa walioangamia. Sehemu ya pili ya makala haya itawajia karibuni.

ALLAH ATUHIFADHI.

(Photo credits  theidealmuslimah.com)

Comments

There are no comments

Post a comment