A PHP Error was encountered

Severity: Notice

Message: Only variable references should be returned by reference

Filename: core/Common.php

Line Number: 272

MAISHA YA ABDILATIF ABDALLAH | Blog
Fun!

Insights

Abdilatif Abdalla alikuwa mwanasiasa na muandishi wa enzi za muanzilishi wa taifa la Kenya Mzee Jomo Kenyatta. Abdilatif alizaliwa mnamo tarehe 14/4/1946 mtaani Kuze mjini Mombasa. Baada ya kushawishiwa na nduguye Sheikh Abdillahi Nassir  ndipo alipoingia katika ulingo wa siasa. Bwana huyu aliweka historia mwaka wa 1969 kwa kuwa mfungwa wa kwanza wa kisiasa baada ya Kenya kupata uhuru wake akiwa na miaka 22 pekee.

Abdilatif  alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na nusu, lakini baada ya aliyekuwa waziri wa sheria wakati huo Charles Njonjo kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo, mahakama iliamua kumuongezea kifungo na kumfunga kwa muda wa miaka mitatu kwa kosa la kuandika  makala aliyoyaita ‘Kenya twendapi?’ Hii ilikuwa nakala ya saba aliyoandika kijana huyu. Humo alishtumu vikali utawala wa rais mwenda zake Mzee Jomo Kenyatta na wote  waliokuwa kwenye mamlaka wakati huo.

Alipokuwa kifungoni katika gereza la Kamiti aliadhibika si haba , kama asemavyo mwenyewe alikua katika ‘gereza ndani ya gereza’ kwani hakuwa na ruhusa ya kutoka wala kuwasiliana na mtu yeyote. Vilevile, hakuwa na ruhusa ya kupewa kalamu wala daftari. Ndani ya gereza, kijana huyu aliwekewa ulinzi wa askari wawili. Kwa bahati nzuri mmoja ya askari hao alikuwa sahiba yake wa karibu. Sahiba huyo alimpa kalamu na daftari licha ya vikwazo vikali vilivyowekwa.  Alitumia muda wake mwingi gerezani kuandika mashairi.

Mwaka wa 1972 mkusanyiko wa mashairi yake ulichapishwa na kitabu kilipewa jina ‘Sauti ya Dhiki’ kilicho haririwa na Shihabudin Chiragdin (Mungu amrehemu). Kitabu hiki kilipata bahati kubwa na alitunikiwa tuzo ya ‘Kenyatta literary award’ mwaka wa 1974. Tuzo hili limeonakana kuwa kinaya kwa wengi. Lugha aliyoitumiya Abdilatif ni ile ya kimvita (Kiswahili cha Mombasa).

Baada ya hapo aliishi uhamishoni na kupokewa na rais wa Tanzania mwendazake Julius Nyerere katika chuo kikuu cha Dar es Salam ambapo alifanya kazi na taasisi ya utafiti wa Kiswahili kwa miaka kadhaa. Alipotoka Tanzania alibahatika kuenda Uingereza na kufanya kazi na shirika la uanahabari la BBC Swahili.  Kama wasemavyo wavyele, “Mwenye lake hawachi,’ AbdiLatif aliendeleza uanaharakati wake wa kutaka kuboresha siasa za Kenya. Hili lilipelekea rais mstaafu Daniel Moi kumtumia watu wawili hadi nchini Uingereza kumshawishi atengane na uanaharakati huku akiahidiwa vinono. Hilo halikumshawishi, na aliendelea na uanaharakati wake.

abdi1

Baadaye alielekea nchini Ujerumani alipoajiriwa kama mhadhiri wa Kiswahili katika Chuo KIkuu cha ZMO.

Kwa wanaomfahamu Abdilatif Abdalla hawatoshangazwa sana kwa ujuzi wa kuandika mashairi yake, labda hii ni kwa ajili ya mazingira aliyoinukia. Maana alizaliwa katika kitovu cha uswahili katika mtaa wa kuze ambako ni mahali alipozaliwa yule shaha wa malenga wa zamani  Muyaka wa Muhaji. Katika familia yake Abdilatif kumetokea washairi akiwemo nduguye Ustadh Ahmad Nassir (Ustadh Bhalo), wasomi, wana siasa kama vile nduguye sheikh Abdillahi Nassir.Vilevile, pia kumetokea waimabaji kama Mohamed Khamis Juma Bhalo (Mungu amrehemu) na hata wapiga ala za kienyeji. Hivi sasa Bwana Adillatif anaishi nchini Ujerumani.

Comments

Gravatar
Ramadhan Yusuf

May 2, 2016

Kwa yakini, Naweza muita ustadh huyu gwiji wa mashairi Abdilatif Abdallaah. Ama kwa hakika Abdilatif Abdallah Kwangu mimi naweza muita mwanzilishi wa ari na hamu yangu ya kujua kutunga na kuhifadhi mashairi yangu mwenyewe, kwa kuwa kupitia kwake, nimeweza kuyatunga mashairi kadh a wa kadha na hata kuweza kuiyachapisha kwa misingi ya kiswahili na usairi bora sana. AMIIIIYN

Post a comment