A PHP Error was encountered

Severity: Notice

Message: Only variable references should be returned by reference

Filename: core/Common.php

Line Number: 272

LENDA ZAKE KUMI LA KWANZA | Blog
Fun!

Insights

KUMI LA KWANZA.

Ramadhani mwezi mwema, ni hunu ushaingia.

Kwenye kumi la rehema, ndilo tunaloanzia.

Sote tufanyeni hima, tupate kujichumia.

Tuchume yalio mema, yaweze tusaidia.

 

Ameyasema Rasuli, kiumbe alio bora.

Kutwambia jambo hili, tupate kuwa imara.

Kwa hakika amefeli, kupata kubwa hasara.

Asisamehewe kweli, naye Illahi Kudura.

 

Ramdhani imwingilie, kwenye siku thalathini.

Kisha asisamehewe, dhambi zake kwa yakini.

Lazima mumuelewe, huyo yuko hasarani.

Ndio nakwambia wewe, tuyashike ya Manani.

 

Tuzidi sana kuswali, na kusoma qur ani.

Tatuhifadhi Jalali, Illahi Ya Rahamani.

Siku hiyo kwa ukweli, tungiyapo Kaburini.

Tutakuwa tu jamali, tupendeze kwa yakini.

 

Tupende sana kutowa, ni jambo lenye thamani.

Ili wapate afuwa, waitwao masikini.

Nao wasilie ngowa, inapofika jioni.

Ili wale sawa sawa, kama wengine jamani.

 

Natowa wangu uneni, Kwanzia kwetu Mombasa.

Tuchumeni tuchumeni, wakati ni hunu sasa.

Labuda hata mwakani, tusifikie kabisa.

Mwezi hunu Ramdhani, mwema wa kututakasa.

 

Ramadhani yapendeza, ni mwezi wenye imani.

Unapata muangaza, ukuwapo ibadani.

Hivyo ninakueleza, fanya hima kwa yakini.

Upate kujiingiza, ufaulu maishani.

 

Kuna mambo ya kishenzi, nawambia ni haramu.

Nayataja wazi wazi, ili mupate fahamu.

Dhumna ni pingamizi, kdhalika na keramu.

Karata zina ajizi, tuwate yaso utamu.

 

Tuuheshimu wakati, kwenye hini Ramadhani.

Tutaona tofauti, kubwa sana kiimani.

Mambo yatakuwa fiti, tufaulu niamini.

Tufikapo kwa mauti, kurudi kwake Manani.

 

Ni kumi lenye Rehema, kutoka kwake Moliwa.

Hivyo tufanyeni hima, kufanya yenye na kuwa.

Kutenda yalio mema, tupate kurehemewa.

Kesho siku ya kiama, tupate kuhifadhiwa.

 

Katika kumi la kwanza, tufanye bidii sana.

Tupate ya muangaza, mambo yenye na maana.

Yale aliyotweleza, Mtume wetu Hashima.

Ili tutoke kwa giza, kwenye Ramadhani njema.

 

Tammati niko mwishoni, mwisho wa shairi langu.

Jina langu Alamini, na Siwa ndiye babangu.

Na Kadara ni mghani, aloghani tungo yangu.

Ni tungo ya Ramadhani, mwisho tumuombe Mungu.

 

(Photo credit myramadan.co.uk)
 

Comments

There are no comments

Post a comment