Insights
Ninatunga nikilia, machozi yatiririka.
Hakika yatukimbia, Ramadhani yatoweka.
Tayari lishaingia, kumi la tatu hakika.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Popote pale ulipo, upate kunisikia.
Zimekwenda ka' upepo, siku zimetukimbia.
Kwa sasa hapa tulipo, la mwisho tushafikia.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Hakika ni sikitisho, yabidi kuvumilia.
Tuko kwa kumi la mwisho, Ramadhani yakimbia.
Tuombeni sahihisho, kutoka kwake Jalia.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Sijui hasa mwakani, kama itatufikia.
Mwezi hunu Ramadhani, mwema unaovutia.
Ni kumuomba Manani, atuhifadhi Jalia.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Kuna tuloanza nao, leo wametupotea.
Wamekwenda njia hiyo, yake Illahi Jalia.
Njia iso kimbilio, sote tutaipitia.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Sisi si werevu wetu, mpaka tukabakia.
Ni uwezo wa Mola wetu, Illahi Mola Jalia.
Ikawa twaitwa watu, bado tuko kwa dunia.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Ramadhani wapendeza, leo unatukimbia.
Wallahi nakueleza, kukuapia Jalia.
Hivyo unavyopenyeza, majonzi watuachia.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Ni kumi hili la Toba, kuomba kusamehewa.
Turudi kwa Mola Rabba, Illahi Mola Moliwa.
Ili tuweke akiba, ya kesho kuitumia.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Tukeshe misikitini, itikafu nawambia.
Tukingia vilioni, kwa Allah kumlilia.
Huruma zake yakini, Allah 'tatuhurumia.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Na usiku wenye cheo, tuhakikishe jamani.
Kwenye kumi hili leo, litupate msikitini.
Na ndio fadhila hiyo, zitukute ibadani.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Jamani tulie sana, Allah kumnyenyekea.
Atusamehe Rabana, Illahi Mola Jalia.
Atupe yenye maana, kesho itapowadia.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Ramadhani ishafika, yaingia kikomoni.
Ibada kuongezeka, wajibu wetu yakini.
Tarawehe kadhalika, yote tuyaongezeni.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Nahisi kama msiba, Ramadhani yaondoka.
Kwa hili kumi la toba, nalo pia lishafika.
Twakuoma Mola Rabba, utupe tunayotaka.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Inanitia shauku, watu kuwa hasarani
Mutembeao usiku, hamutoki madukani.
Si vyema kuenda huku, Ramadhani i mwishoni.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Wazazi tusikubali, mabinti kutoka toka.
Mabarobaro kwa kweli, nao wao kuzunguka.
Tuhakikishe kwa hili, msikitini wamefika.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Tuwapeni muongozo wana wetu nawambia.
Wasipate ya muozo, siku inapowadia.
Ili wakapate tuzo, badala ya kujutia.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Matozi yabubujika, siilengi mistari.
Ninashindwa kuandika, inatwambia kwaheri.
Ramadhani yaondoka, yarudi kwake Kahari.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Sijui tutaikuta, itapofika mwakani.
Twaomba bila kusita, kutoka kwake Manani.
Atupe kumeremeta, pepo yenye na thamani.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Ya Rabbi tukubalie, funga zetu kwa yakini.
Na pia tuhurumie, tusamehe Ya Manani.
Illahi tufikirie, sisi ni viumbe duni.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Yabidi kulifupisha, kulifikisha kikomo.
Mtunzi nawajulisha, Jina Alamin Somo.
Nawaombea maisha, tupate ya msimamo.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
MALENGA WA MOMBASA
ALAMIN S.SOMO
MOMBASA
24.06.2014
(Photo credit muslimvillage.com)
Hakika yatukimbia, Ramadhani yatoweka.
Tayari lishaingia, kumi la tatu hakika.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Popote pale ulipo, upate kunisikia.
Zimekwenda ka' upepo, siku zimetukimbia.
Kwa sasa hapa tulipo, la mwisho tushafikia.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Hakika ni sikitisho, yabidi kuvumilia.
Tuko kwa kumi la mwisho, Ramadhani yakimbia.
Tuombeni sahihisho, kutoka kwake Jalia.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Sijui hasa mwakani, kama itatufikia.
Mwezi hunu Ramadhani, mwema unaovutia.
Ni kumuomba Manani, atuhifadhi Jalia.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Kuna tuloanza nao, leo wametupotea.
Wamekwenda njia hiyo, yake Illahi Jalia.
Njia iso kimbilio, sote tutaipitia.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Sisi si werevu wetu, mpaka tukabakia.
Ni uwezo wa Mola wetu, Illahi Mola Jalia.
Ikawa twaitwa watu, bado tuko kwa dunia.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Ramadhani wapendeza, leo unatukimbia.
Wallahi nakueleza, kukuapia Jalia.
Hivyo unavyopenyeza, majonzi watuachia.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Ni kumi hili la Toba, kuomba kusamehewa.
Turudi kwa Mola Rabba, Illahi Mola Moliwa.
Ili tuweke akiba, ya kesho kuitumia.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Tukeshe misikitini, itikafu nawambia.
Tukingia vilioni, kwa Allah kumlilia.
Huruma zake yakini, Allah 'tatuhurumia.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Na usiku wenye cheo, tuhakikishe jamani.
Kwenye kumi hili leo, litupate msikitini.
Na ndio fadhila hiyo, zitukute ibadani.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Jamani tulie sana, Allah kumnyenyekea.
Atusamehe Rabana, Illahi Mola Jalia.
Atupe yenye maana, kesho itapowadia.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Ramadhani ishafika, yaingia kikomoni.
Ibada kuongezeka, wajibu wetu yakini.
Tarawehe kadhalika, yote tuyaongezeni.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Nahisi kama msiba, Ramadhani yaondoka.
Kwa hili kumi la toba, nalo pia lishafika.
Twakuoma Mola Rabba, utupe tunayotaka.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Inanitia shauku, watu kuwa hasarani
Mutembeao usiku, hamutoki madukani.
Si vyema kuenda huku, Ramadhani i mwishoni.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Wazazi tusikubali, mabinti kutoka toka.
Mabarobaro kwa kweli, nao wao kuzunguka.
Tuhakikishe kwa hili, msikitini wamefika.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Tuwapeni muongozo wana wetu nawambia.
Wasipate ya muozo, siku inapowadia.
Ili wakapate tuzo, badala ya kujutia.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Matozi yabubujika, siilengi mistari.
Ninashindwa kuandika, inatwambia kwaheri.
Ramadhani yaondoka, yarudi kwake Kahari.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Sijui tutaikuta, itapofika mwakani.
Twaomba bila kusita, kutoka kwake Manani.
Atupe kumeremeta, pepo yenye na thamani.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Ya Rabbi tukubalie, funga zetu kwa yakini.
Na pia tuhurumie, tusamehe Ya Manani.
Illahi tufikirie, sisi ni viumbe duni.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
Yabidi kulifupisha, kulifikisha kikomo.
Mtunzi nawajulisha, Jina Alamin Somo.
Nawaombea maisha, tupate ya msimamo.
Ramadhani watoweka, unaniwacha na nani.
MALENGA WA MOMBASA
ALAMIN S.SOMO
MOMBASA
24.06.2014
(Photo credit muslimvillage.com)
There are no comments