A PHP Error was encountered

Severity: Notice

Message: Only variable references should be returned by reference

Filename: core/Common.php

Line Number: 272

KUMI LA PILI | Blog
Fun!

Insights

Ramadhani yenda zake, taratibu yatoweka.
 
Jamanini tupulike, hili tupate kumbuka.
 
Yalo mema tuyashike, kuyafuata haraka.
 
Ili moto tu'wepuke, tupate kusitirika.
 
 
 
Sasa ni kumi la pili, ni kumi la Maghfira.
 
Ni hili lishawasili, la kwanza lishatugura.
 
Hivyo nawambia kweli, tufanye yalio bora.
 
Tufanye njema amali, kesho tupate kung'ara.
 
 
 
Nawapa yenye faraji, japo yanasikitisha.
 
Limekwenda kama maji, kumi la kwanza 'mekwisha.
 
Tumuombeni Mpaji, Illahi kutuwezesha.
 
Atupe yenye na taji, taji jema kutuvisha.
 
 
 
Walokuwa wamelala, nawambia waamke.
 
Tufanyeni hala hala, tusiwate iondoke.
 
Bila kupata fadhila, Illahi kutoka kwake.
 
Atujalie jamala, na kesho tusitirike.
 
 
 
Kwisha limeshaondoka, kumi la kwanza wenzangu.
 
Wallahi twahuzunika, ela ni amri ya Mungu.
 
Tufanye yenye baraka, tusipate ya tewengu.
 
Pindi ikimalizika, turidhie Bwana Mungu.
 
 
 
Kabisa tusikubali, tukabaki nyuma nyuma.
 
Tufanye njema amali, kwa kuchuma mambo mema.
 
Yale ya Tumwa Rasuli, Mtume wetu Hashima.
 
Kwa ili tuwe jamali, atuhifadhi Karima.
 
 
 
Sana ninahuzunika, na kutamani kulia.
 
Kumi la kwanza hakika, kwisha lishatukimbia.
 
Tumuombeni Rabuka, Illahi Mola Jalia.
 
Atupe tunayotaka, amali kuziridhia.
 
 
 
Illahi Muumba mbingu, Ramadhani yatugura.
 
Kumi la pili kwa fungu, liitwalo maghfira.
 
Nakuomba Mola wangu, utupe njema bishara.
 
Tusameheme bwana Mungu, kesho tupate kung'ara.
 
 
 
Sasa ninajibambanya, kwa sana kuwakumbusha.
 
Kwa sote tulio kenya, tupate jikurubisha.
 
Kwake Illahi Rabana, Mola mwenye kuwezesha.
 
Ili tukapate Janna, Fir-daus nawajulisha.
 
 
 
Ramadhani kwa kweli, ni hini inayoyoma.
 
Tuko kwa kumi la pili, tufanyeni hima hima.
 
Kufanya njema amali, atuhifadhi Karima.
 
Illahi Mola Jalali, kesho siku ya kiama.
 
 
 
Mwisho niko kwa kikomo, naweka kalamu chini.
 
Jina Alamini Somo, nilotunga tungo hini.
 
Na Kadara pia yumo, kwa hakika ni mghani.
 
Tuombeni msimamo, kwenye hini Ramadhani.
 
 
 
MALENGA WA MOMBASA
 
Alamin S.Somo
 
Mombasa
 
24.06.2014
 
 
 
 
 
(Photo credit muslimvillage.com)


Comments

There are no comments

Post a comment