A PHP Error was encountered

Severity: Notice

Message: Only variable references should be returned by reference

Filename: core/Common.php

Line Number: 272

HABARI KWA UFUPI-7 | Blog
Fun!

Current Affairs

Mshukiwa wa ugaidi afanikiwa kukwepa mtego wa polisi eneo la Mkwajuni kaunti ya Kwale. Hatahivyo, polisi walinasa grinedi moja, risasi 78 na viatu vya polisi. Haya yanajiri siku moja baada ya mauaji ya watu wanne eneo la Likoni, Mombasa.

Washukiwa wanne wa ujambazi akiwemo mwanamke mmoja wauawa mtaani Parklands jijini Nairobi.

Idara ya Mawasiliano ya Ikulu (PSCU) yakanusha uvumi kuwa rais mstaafu Mwani Kibaki amefariki. Kupitia mtandao wa Twitter idara hiyo: “Rais mstaafu Mwai Kibaki yuko hai na buheri wa afya, habari hizo nyingine zinazozunguka mtandaoni ni uvumi mtupu."

Anwani ya jeshi la Kenya KDF katika mtandao wa kijamii wa Twitter wavamiwa. Aliyetekeleza hilo, anaandika jumbe za kukashifu KDF pamoja na serikali ya Kenya.

Mahakama yasitisha agizo la waziri wa Leba Kazungu Kambi la kuwasimamisha kazi katibu mkuu wa muungano wa wafanyikazi COTU Francis Atwoli na Katibu Mkuu Mtendaji wa Shirikisho la Waajiri nchini FKE Jackline Mugo kama wanachama wa bodi ya NSSF.

Inspektaa Jenerali wa polisi David Kimaiyo alegeza marufuku ya kutembea kati ya 6.00pm na 6.00am aliyoiweka katika kaunti ya Lamu. Haya yanajiri baada ya mkutano wa viongozi wa kiislamu.

Waziri wa elimu Prof Jacob Kaimenyi ameagiza walimu wakuu wa shule zote za upili za umma kuwakabidhi wanafunzi waliokuwa na madeni ya karo vyeti vyao.

Comments

There are no comments

Post a comment