A PHP Error was encountered

Severity: Notice

Message: Only variable references should be returned by reference

Filename: core/Common.php

Line Number: 272

HABARI KWA UFUPI 17/7 | Blog
Fun!

Current Affairs

Serikali imepewa mwezi mmoja kukamilisha uchunguzi wake dhidi ya gavana wa Lamu Isaa Timamy. Wakili wa serikali hapo jana aliomba mahakama muda zaidi wa miezi miwili. Timay anakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya zaidi ya watu 60 Mpeketoni kaunti ya Lamu.

Wanaume watatu wamepatikana wakiwa wameuawa na sehemu zao za siri kunyofolewa kwenye barabara kuu ya Embu kuelekea Mwea kaunti ya Kirinyaga. Afisa mkuu wa upelelezi eneo hilo alisema uchunguzi unaonesha jamaa hao waliteswa kabla kuuawa.

Wanajeshi wa Kenya watasalia Somalia hadi pale Muungano wa Afrika
(AU) ama serikali ya Somaliaitakapowaamrisha kuondoka. Haya ni kwa muujibu wa wakuu wa kamati mbili za bunge zinazohusu usalama na ulinzi.

Mwenyekiti wa kamati ya Usalama wa Kitaifa Asman Kamama pamoja na mwenzake wa
Ulinzi na Masuala ya Kitaifa Bw Ndungu Gethenji wameomba muungano wa CORD kutolitia siasa suala hilo.

Wanasiasa wawili wa zamani ni miongoni mwa watu wanaotarajiwa kuhojiwa kwa nafasi za makamishna katika tume ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa (NCIC). Wawili hao ni aliyekuwa spika wa bunge Francis Ole Kaparo na aliyekuwa waziri wa utalii Morris Dzoro

Comments

There are no comments

Post a comment