Current Affairs
HABARI KWA UFUPI
Mwanamume mmoja mwenye umri wa makamu alijirusha kutoka ghorofa ya nne mtaani Mwembe Kuku mjini Mombasa baada ya ugomvi wa kinyumbani.
Mahakama kuu jijini Nairobi imetupilia mbali ombi la seneta wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko la kutaka kusitisha mkutano wa Saba Saba utakaoandaliwa na CORD siku ya Jumatatu katika uwanja wa Uhuru Park.
Zaidi ya polisi 15,000 kutumika katika kuboresha usalama jijini Nairobi wakati wa mkutano wa Saba Saba Uhuru Park siku ya Jumatatu.
Serikali yaanzisha uchunguzi wa matumizi ya fedha za umma wakati wa ziara za wawakilishi wa wadi kote nchini.
There are no comments