Current Affairs
GAVANA wa Lamu Issa Abdalla Timamy pamoja na Kamishna wa Kaunti, Bw Miiri Njenga, Jumatano waliandaa mkutano wa dharura na wananchi ili kuwaondolea wasiwasi ambao hadi sasa umepelekea wakazi wengi kuhama mji wa Lamu na viungani mwake.
Wakaazi wengi mjini humo wameamkia safari kurudi makwao kufuatia vijikaratasi vilivyosambazwa mnamo Jumanne asubuhi vilivyoonekanaa kuwalenga watu wa dini moja ya Wakristo.
Vijikaratasi hivyo vilidai kuwa magaidi walikuwa wamechoshwa na Wakristo na serikali ya Kenya ambayo kila mara huwatesa na kuwadhalilisha waislamu na kwamba tayari magaidi walikuuwa Lamu kutekeleza shambulizi.
Kufuatia onyo hilo, imemlazimu Gavaana Timamy kuwekaa wazi kwa wananchi wake kwamba kamwe hakuna ubaguzi wa kidini wala kikabila katika kaunti ya Lamu.
SERIKALI imekiri kuna shida katika shule za upili kutokana na kucheleweshwa kwa utoaji wa pesa za elmu ya bure kwa shule za upili za kutwa.Walimu wakuu wameonya huenda wakalazimika kufunga shule kutokana na hali iliyopo.Walitoa wito serikali itoe pesa hizo haraka iwezekanavyo na kusema hawana uwezo wa kulisha watoto na kulipa wafanyakazi.
MAHAKAMA ya Juu yamrudisha kazini Gavana wa Garissa Nathif Jama Adam ilipotupilia mbali uamuzi wa Mahakama ya rufaa kwamba uchaguzi katika kaunti hiyo urudiwe.
Majaji Dkt Willy Mutunga , Kalpana Rawal, Philip Tunoi, Jackton Ojwang, Mohammed Ibrahim, Njoki Ndungu na Smokin Wanjala waliikosoa mahakama ya rufaa kwa kutoa maamuzi tofauti kuhusu kesi za uchaguzi kutoka kaunti hiyo.
Majaji hao walikubaliana na Jaji Alfred Mabeya wa Mahakama kuu aliyeamua Bw Adam alikishinda kiti hicho kwa njia halali. Bw Adam aliyechaguliwa kwa tikiti ya chama cha Wyper alitangazwa mshindi na msimamizi wa uchaguzi kaunti ya Garissa baada ya kupata kura 37,910.
Mpinzani wake wa karibu Bw Ali Bunow Korane alimfuata kwa karibu alipopata kura 35,098. Baada ya kutangazwa mshindi wapiga kura wawili Mabw Abdikharim Osman Mohammed na Sahel Nuno Abdi waliwasilisha kesi wakipinga matokeo hayo ya uchaguzi.
MAHABUSU aliyetoroka akiwa na pingu akipelekwa hospitali kutibiwa alishangaza mahakama aliposema kwamba hajui alivyofanya hivyo, akidai yeye ni mfungwa mwenye nidhamu.
George Morara Bosire alisema kwamba anatambuliwa kama mahabusu mwenye nidhamu katika jela la Nairobi West na hajui kilichomfanya kutoroka akiwa hospitali kuu ya Kenyatta.

There are no comments