A PHP Error was encountered

Severity: Notice

Message: Only variable references should be returned by reference

Filename: core/Common.php

Line Number: 272

HABARI KWA UFUPI 2/7/14 | Blog
Fun!

Current Affairs

news in short copyWatu 4 wafariki baada ya ndege ya kubebea mizigo walimokuwa wakisafiria kuanguka mtaani Utawala eneo bunge la Embakasi jijini Nairobi. Ndege hiyo ilikuwa ikisafirisha miraa kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta kuelekea Mogadishu nchini Somalia.

Dereva wa mojawapo ya magari yaliyotumiwa na wavamizi wa mpeketoni alifikishwa katika mahakama kuu mjini Mombasa na kufunguliwa mashtaka ya mauaji ya Zaidi ya watu 12. Hatahivyo, Dyana Salim alikanusha mashtaka hayo. Dyana anadai kuwa alitekwa nyara na wavamizi hao na kupokonywa gari lake kabla ya wao kutekeleza mauaji hayo. Kesi yake itasikilizwa tena siku ya Jumatatu.

Inspekta Jenerali wa polisi David Kimayo awaamuru makamishna wa kaunti zote kuboresha usalama wakati wa mkutano wa kisiasa uliyopangwa na upinzani maarufu kama saba saba.

Mawaziri  wa afya kutoka nchi tofauti za Afrika wakutana jijini Accra huko Ghana kwa kikao cha dharura kinachotazamiwa kujadili mkurupuko wa maradhi ya ebola nchini Guinea, Liberia na Sierra Leone. Kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) kufikia sasa kumeripotiwa visa 759 vya maambukizi.

Comments

There are no comments

Post a comment