Current Affairs
CHAMA cha Kitaifa cha Walimu (Knut) kimetishia kuitisha mgomo ikiwa
makamishna wa Tume ya Kuajiri Walimu (TSC) hawatakuwa wameteuliwa
katika kipindi cha siku saba zijazo.
Knut pia ilionya Wizara ya Elimu dhidi ya kushirikiana kisiri na wakurugenzi wa
elimu katika kaunti kuunda sheria ambazo zitakandamiza walimu.
MAELEZO ya kushangaza yameibuka kuhusu namna wavamizi walioshambulia
vijiji vya Pandanguo na Jima mnamo Jumamosi usiku walikuwa na ujasiri kiasi
kwamba waliingia msikitini na kuhubiri kwa dakika 30.
Isitoshe, wahalifu hao baadaye walivamia shamba la mmoja wa wakazi wa
sehemu hiyo na kuvuna mahindi mabichi kisha kuondoka tararibu.
Yote hayo yalifanyika licha Serikali kutoa hakikisho kwa wakazi wa sehemu hiyo kuwa usalama ulikuwa umeimarishwa kufuatia kupelekwa kwa vikosi tofauti
vya usalama kushika doria katika eneo zima la Lamu.
POLISI wanachunguzwa kufuatia madai ya kuhangaisha, kupokea hongo na
kutumia nguvu kupita kiasi wakati wa operesheni ya 'Usalama Watch’ iliyofanywa katika mtaa wa Eastleigh, Nairobi iliyolenga kukabiliana na
washukiwa wa ugaidi nchini.
Mwenyekiti wa Mamlaka huru ya kusimamia polisi (Ipoa) Bw Macharia Njeru,
alisema walifanya uchunguzi wao kibinafsi na kutambua kuna polisi 29
wanaofaa kushtakiwa punde baada ya madai hayo kuthibitishwa.
Bw Njeru alisema wamepata kuwa polisi waliohusika kwenye operesheni hiyo waliitisha hongo ya kati ya Sh1,000 na Sh20,000 huku kukiwa pia na malalamishi kuwa, wafungwa walipigwa walipokamatwa na katika vituo vya polisi.
Akizungumza Nairobi alipozindua ripoti kuhusu operesheni hiyo, alisema shirika hilo limeagiza idara ya huduma za polisi wa kitaifa ianzishe uchunguzi mara
moja kuhusu madai hayo pamoja na yale kuhusu ufisadi wa polisi haraka
iwezekanavyo.
KESI ya pili ya uhalifu inayomkabili polisi bandia Joshua Waiganjo
imeondolewa katika mahakama ya Nairobi. Bw Waiganjo aliachiliwa bila masharti baada ya shahidi wa upande wa mashtaka kukataa kufika mbele ya mahakama hiyo.
RAIA wa Uingereza anaiomba Mahakama Kuu imsukume gerezani afisa mkuu
katika idara ya uhamiaji kwa kukaidi agizo la Mahakama apewe kibali cha
kufanya kazi humu nchini.

There are no comments