A PHP Error was encountered

Severity: Notice

Message: Only variable references should be returned by reference

Filename: core/Common.php

Line Number: 272

HABARI KWA UFUPI 14/7 | Blog
Fun!

Current Affairs

Gavana wa Mombasa Hassan Ali Joho ametishia kuchukua magari aliyokuwa amewapa polisi watumie kuimarisha usalama wa kaunti hiyo kwa madai kuwa yanatumiwa vibaya. “Ukinichezea nitachukua magari niliyoyafadhili kwa idara ya usalama na kuyapeana kwa serikali ya kaunti niyapake rangi na kuwapatia askari wa kaunti ." Alisema Joho.

Shinikizo zazidi kutolewa kwa rais Uhuru Kenyatta za kumtaka amfute kazi waziri wa usalama wa ndani Joseph Ole Lenku hii ni baada ya chama cha TNA kinachoongozwa na rasi Uhuru kudai utendakazi wa Lenku sio wa kuridhisha. Haya yanajiri baada ya mashambulizi kadhaa yaliopelekea vifo vya watukutokea  katika kaunti za Lamu na Tana River.

Mashambulizi mengine yaripotiwa katika kijiji cha Pandanguo eneo la Witu. Waliotekeleza mashambulizi hayo waliiba mali za wenyeji ikiwemo mahindi yaliyokuwa yanasubiri kuvvunwa.

Hoteli maarufu ya Ras Kitau yateketea moto na kusababisha hasara ya thamani kubwa usiku wa kuamkia leo katika kaunti ya Lamu. Chanzo cha moto huo hakijajulikana.

Mtoto wa darasa la nne amepatikana akiwa amelewa chakari hadi kuzirai katika eneo la Kitengela. Inadaiwa kijana huyo wa miaka kumi alishawishiwa na jamaa mmoja wa umri wa makamu kutumia pombe hiyo.

Comments

There are no comments

Posting comments after has been disabled.