A PHP Error was encountered

Severity: Notice

Message: Only variable references should be returned by reference

Filename: core/Common.php

Line Number: 272

HABARI KWA UFUPI 24/7/14 | Blog
Fun!

Current Affairs

Mwanamume wa umri wa miaka 29 leo aliwekwa chini ya ulinzi mkali katika hospitali ya Tigoni, Limuru ambako amelazwa kwa madai kuwa aliua mpenzi wake kisha akajaribu kujiua.

WANAFUNZI wawili walifariki na mwengine akajeruhiwa baada ya kupigwa na radi katika kaunti ya Nandi. Wanafunzi hao wa shule ya upili ya AIC Kemel eneo la Kipkaren, Nandi Kaskazini, walikuwa kwenye uwanja wakicheza walipopigwa na radi mwendo wa saa kumi alasiri siku ya Jumatano.

WAHUDUMU wa matatu wamepata afueni baada ya gavana wa Nairobi, Dkt Evans Kidero kuagiza ada ya kuegesha magari ipunguzwe. Punguzo hilo linalenga matatu ambazo zimesajiliwa kwenye takriban vyama 70 vya ushirika (Saccos) na litaanza kutekelezwa mwezi ujao.

CHAMA cha TNA kimeanzisha kampeni ya kuwasajili vijana walio chini ya umri wa miaka 18 kama wanachama kote nchini.Usajili huo ulizinduliwa Alhamisi katika kaunti ya Nyeri na katibu mkuu wa chama hicho Bw Onyango Oloo.

Comments

There are no comments

Post a comment