Current Affairs
Mmiliki wa kampuni ya mabasi ya usafiri ya Modern Coast Shahid Butt auwawa kwa kupigwa risasi ndani ya gari lake na watu wasiojulikana eneo la Changamwe kaunti ya Mombasa. Mauaji haya yanajiri hata baada ya serikali kuhakikishia Wakenya usalama. Butt aliwahi kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kufadhili vijana wenye misimamo mikali.
Familia moja mjini Mombasa yadai polisi walimpiga risasi mwana wao mwenye umri wa miaka 4 wakati wa mauaji ya Butt. Mtoto huyo amekatwa mguu na kwa hivi sasa amelazwa katika hospitali ya Bomu.
Rais Uhuru Kenyatta asisitiza kuwa yuko tayari kwa majadiliano na yeyote aliye na mawazo ya kuendeleza nchi. Rais ashtumu upinzani akisema unakwamisha utekelezaji wa mipango ya maendeleo na utoaji wa huduma bora kwa Wakenya.
Tume ya usawazishaji mishahara na marupurupu (SRC) imetishia kufutilia mbali marupurupu ya wawakilishi wa wadi iwapo wataendelea kufuja pesa za umma.
Sekta ya utalii kisiwani Lamu imeathirika pakubwa tangu machafuko ya Mpeketoni na viungani mwake. .Zaidi ya watu themanini(80) wamepoteza maisha na mali ya thamani isiyojulikana kuteketezwa.
Mahakama ya rufaa jijini Nairobi yaamuru Shirika la Ndege la Kenya Airways (KQ) iwalipe wafanyakazi wapatao 447 mishahara ya miezi sita kwa kuwafuta kazi kwa njia isiyo halali.

There are no comments