Fun!

Current Affairs

WATU saba akiwemo chifu, afisa wa Afya ya Umma na walimu wawili wafariki katika kaunti ya Nandi kwa kunywa pombe iliyokuwa na sumu.Kati ya hao,wawili walifariki katika nyumba zao huku watano wakikata roho wakiwa katika hospitali ya Rufaa ya kaunti ya Kapsabet waliokuwa wamepelekwa.

WANAWAKE watano na mwanaume mmoja washtakiwa kwa wizi wa mtoto mchanga waliyenuia kumuuza katika kijiji cha Soweto mtaani Kayole kaunti ya Nairobi. Waliofikishwa mbele ya hakimu mkazi katika Mahakama ya Milimani Nairobi Bw Joseph Karanja na Hellen Mutile (Judy Wairimu, Bw Dickson Maina, Penninah Kerubo, Sarah Ambiyo na Lilian Wanjiru).Washukiwa hao wataendelea kukaa rumande hadi kesi itakapo endelea kusikizwa.

WATOTO watano wa kipalestina ni miongoni mwa watu 21 waliouwawa katika mashambulizi ya angani yanayofanywa na Israel katika ukanda wa Gaza, hii ni kulingana na wataalamu wa afya katika ukanda huo.kufikia sasa idadi ya walio fariki imeongezeka themanini(80) tangu Israel ilipoanzisha mashambulizi ya angani siku
ya Jumanne, dhidi ya Gaza.

Comments

There are no comments

Post a comment