Current Affairs
MBUNGE wa Lungalunga Khatib Mwashetani na Mwakilishi wa wanawake
katika kaunti ya Kwale Zainab Chidzuga wamepuuzilia mbali madai ya
viongozi kutoka mrengo wa CORD kuwa wao ni wasaliti kwa kutangaza wazi
msimamo wao wa kufanya kazi na serikali.
Kauli ya viongozi hao imejiri siku chache tu baada ya matamshi hayo kutolewa
katika hafla ya Iftar ambayo ili hudhuriwa na kinara wa mrengo wa CORD Raila
Odinga katika kaunti ya Mombasa wiki iliyopita.
GAVANA Okoth Obado wa Migori Ijumaa alichinja fahali 50 kusherehekea
ushindi wa kurudishiwa kiti hicho na Mahakama ya Juu.
Siku moja baada ya kutangazwa mshindi halisi wa kiti hicho cha Ugavana
Migori Bw Obado alitembelea maeneo mbali mbali kuwafahamisha wananchi
tukio hilo.Gavana huyo alikuwa na msafara wa magari zaidi ya
100 alipozuru Rongo, Ranen, Awendo, Uriri, Migori na Isebania.Alisimama katika vituo mbali mbali kupokea salamu kutoka kwa wananchi.
MBUNGE wa Nandi Hills Alfred Keter amesema kwamba masuala yaliyotolewa
na Muungano wa Cord ni masuala halali na serikali lazima iyajibu ili kulinda
maisha ya Wakenya. Akizungumza katika majengo ya Bunge , Bw Keter alisema serikali lazima ipatie uzito masuala hayo ili kuzuia mzozo nchini.
MALUMBANO kati ya Waziri wa Leba Kazungu Kambi na katibu mkuu wa
muungano wa vyama vya wafanyakazi nchini COTU Francis Atwoli huenda
yakaendelea kukithiri baada ya waziri huyo kumstaafisha Atwoli kama
mwanachama wa bodi wadhamini ya hazina ya malipo ya uzeeni.
Mapema Ijumaa Waziri Kambi alipotangaza hatua hiyo ambapo pia mkurugenzi
mkuu wa chama cha waajiri, FKE Bi Jacquelinie Mugo alistaafishwa, alinukuu
sheria mpya ya NSSF iliyoanza kutekelezwa kuanzia Aprili mwaka huu,
inayopiga marufuku mwanachama yeyote kuhudumu zaidi ya miaka sita.
NDEGE ya Malaysia iliyotunguliwa katika eneo linalodhibitiwa na waasi
mashariki mwa Ukraine ilikuwa ikipaa katika himaya ambayo kampuni zingine
za ndege barani Asia zilikuwa zimeacha kutokana na hofu za kiusalama.
Kampuni mbili za ndege nchini Korea Kusini, Korea Air na Asiana, kampuni ya Qantas kutoka Australia na China Airlines kutoka Taiwan zilisema kuwa zilikuwa
zimebadilisha njia hiyo kuanzia mwezi Machi baada ya majeshi ya Urusi kufika eneo la Crimea.

There are no comments