A PHP Error was encountered

Severity: Notice

Message: Only variable references should be returned by reference

Filename: core/Common.php

Line Number: 272

FAIDA ZA SWALA YA USIKU (QIYAAM). | Blog
Fun!

Life Style

Mwenye kuswali Qiyaamul-layl:

1.Hupata siha katika mwili.

Amesema mtume (Swalla Allahu Alaihi wa Sallam): “Shikamaneni na kusimama (kuswali) usiku kwani ni tabia/adabu za waja wema kabla yenu, na kujikurubisha kwa Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) na ni kafara ya maovu, na ni kinga ya dhambi, na ni kinga yaa maradhi katika mwili.” [Ahmad na At-Tirmidhiy na kaisahihisha Shaykh Al-Albaaniy].

2.Hukubaliwa du'aa haraka

Amesema Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi wa Aalihi wa Sallam): “Hakika katika usiku kuna saa ambayo mja anapomuomba Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) kheri katika mambo ya dunia au akhera ila (Allah) Humpa kheri hizo, na hivyo ni kila usiku.” [Muslim].

3.Hupata utukufu mja 

Amesema mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi wa Aalihi wa Sallam): “Amenijia Jibril akasema: Ewe Muhammad ishi upendavyo bila shaka wewe ni maiti (utakufa), na mpende umtakaye bila shaka utafarikiana naye, na tenda unavyopenda lakini ujue utalipwa kwa vitendo hivyo, na tambua kwamba utukufu wa Muumin ni Qiyaamul-Llayl, na heshima yake ni kujitosheleza na watu.” [Al Haakim na Al Bayhaqiy, na Al Mundhiriy na Al-Albaaniy wamesema ni Hadiyth Hasan

4. Humpelekea mja kupata husnul-khaatimah (mwisho mwema)

Amesema Mtume (Swalla Allahu Alaihi wa Sallam): “Atakayesimama (usiku) na ayah kumi hatoandikwa miongoni mwa walioghafilika, na atakayesimama kwa ayah mia ataandikiwa ni miongoni mwa wanyenyekevu, na atakayesimama kwa ayah elfu ataandikwa miongoni mwa wenye thawabu nyingi (mwenye mrundi wa thawabu).” [Abu Dawuud na amesahihisha Shaykh Al-Albaaniy].

Ndugu wa Kiislamu, kama tulivyoona faida na fadhila nyingi za swala za usiku ni juu yetu. Sasa kujihimiza katika kutekeleza ibada hii yenye fadhila nyingi. Na ili iwe rahisi kwetu na wepesi kuitekeleza ibada hii ni muhimu kuzingatia yafuatayo :

i. Usile na kunywa hadi ukashiba sana usiku.
ii. Usijitaabishe sana mchana kwa yasiyo na faida.
iii. Usiache kulala kidogo mchana kwani inasaidia kuamka usiku.
iv. Usifanye maasi kwani yanamzuia mtu kuamka Qiyaamul- layl.
v. Safisha moyo wako kutokana na uhasidi, chuki na waislamu wenzako.
vi. Fikiria mauti na usiwe na matumaini ya kuishi sana.
vii. Tambua fadhila zake.

Tunamuomba Allah (Subuhanahu wa ta‘ala) atuwafikishe katika kusimama usiku pamoja na kutekeleza ibada nyengine za kheri na atukubalie amali zetu zote na atuingize katika Pepo yake pamoja na waja wake wema. Amin

Comments

There are no comments

Post a comment