A PHP Error was encountered

Severity: Notice

Message: Only variable references should be returned by reference

Filename: core/Common.php

Line Number: 272

World cup vs Ramadhan | Blog
Fun!

Insights

 
 

TUSIHADAIWE...


 

Leo tarehe 12 mwezi Juni dimba la kombe la dunia (World Cup) linang'oa nanga jijini Sao Paolo nchini Brazil. Ulimwengu mzima una hamu ya kutazama dimba hili linalotazamiwa kuwa na mhemko si haba...

Hatari ya dimba hili kwa Waislamu ni kuwa wengi wetu tunajisahau na kuanza kupuuza ibadah.

Dimba hili litaendelea hadi tarehe 13 mwezi Julai, yani kwa kipindi cha mwezi mzima. Mwezi mtukufu wa Ramadhan nao unabisha hodi na unatarajiwa kuanza pengine tarehe 28 mwezi huu. Ina maana 'World Cup' itaendelea kwa kipindi cha siku 15 za Ramadhan. Mwezi ambao una umuhimu mkubwa kwa Waislamu.

(شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنْزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ... )

'Mwezi wa Ramadhan ambao iliteremshwa humo Qur'an kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi...'

Baqarah 185

Mwezi ambao Jibril 3aleihi Ssalaam,, mwaminifu wa mbingu saba, alikuwa akishuka na kuja kusoma Qur'an na Mtume Muhammad SwallALLAHu 3aleihi Wa Ssalaam....

Mechi moja ya mpira huwa na dakika si chini ya 90. Ikiwa siku 15 za Ramadhan tutaziharibu kwa 'World Cup' basi ina maana tutapoteza dakika si chini ya 1350 za kufanya ibadah kwa mechi moja kwa siku. Kumbuka kwa siku kuna mechi zaidi ya moja. Tutakuwa ni waja wenye faida iwapo dakika hizi tutazitumia kwa kujikurubisha kwa ALLAH kwani Ramadhan imeletwa ili tukuze imaan zetu na tuwe wacha Mungu zaidi..

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ)

'Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu'

Baqarah 183

Wallahy 'World Cup' haitotuingiza peponi na wala haitotukurubisha kwa ALLAH!

Mwaka huu (1435/2014) ni mwaka wa fitnah na ni mwaka wa kupima imani zetu kama Waislamu. Tazama ratiba ya mechi za 'World Cup' utagundua kuwa mechi ya kwanza ya siku huanza mwendo wa saa moja jioni (7pm). Wakati ambao watu watakua miskitini kwa swalah ya Maghrib na baadae kuenda majumbani na kujumuika na familia kwa iftaar.

Wengi wetu tutasahau umuhimu wa kujumuika na familia zetu kwa iftaar kwa kigezo kuwa hatutaki kupitwa na mechi na hapa kuna sababu za uhusiano wa  kifamilia kudhoofika na baadhi ya familia kuvunjika kwa kuwa watu wataifanya 'World Cup' kuwa na umuhimu zaidi.

Mechi hii itaendelea hadi wakati wa swalah ya Ishaa na kuanza kwa taraweh. Itakapo kwisha, mechi ya pili iliyoratibiwa kuanza saa nne usiku (10pm) itakuwa inakaribia kuanza. Hapa utamu wa mechi ya kwanza utakua umekolea na hamu ya mechi ya pili itakua imetushika. Kwa udhaifu wetu, tutasahau na kupuuza swalah ya Ishaa pamoja na Taraweh.

Mechi ya tatu itakuwa saa saba usiku (1am), wakati ambao Waislamu wanatarajiwa kukithirisha Ibadah. Usisahau kuwa kulala ni miongoni mwa Ibadah. Mechi hii itaendelea hadi saa tisa usiku (3am). Utakapo kwenda kulala utakua ni mwingi wa hasara na machofu. Suala ya usiku (Tahajjud) na Swalah ya Fajr zaweza kukupita kwa machofu..

Utakapoamka mbio maskani kwenda kuzungumzia kuhusu michuano ya jana badala ya kutumia m'da huo kuleta dhikri.

Wangapi wanatamani wangelikua hai angalau kushuhudia Ramadhani hii? Wangapi wanatamani wangelikua na afya ya kuweza kufunga Ramadhani hii?

Tukumbuke na aya hii:

(أَيَّامًا مَعْدُودَاتٍ ۚ... )

'(Mfunge) siku maalumu za kuhesabika..'

Baqarah 184

Chaguo ni letu. Ramadhan ambayo ni siku chache za kutukurubisha zaidi kwa ALLAH ama 'World Cup' ambayo itatuletea hasara hapa Duniani na kesho Akhera.

ALLAH atuongoze na atujaalie tuwe sababu ya wengine kuongoka.

Comments

There are no comments

Post a comment