A PHP Error was encountered

Severity: Notice

Message: Only variable references should be returned by reference

Filename: core/Common.php

Line Number: 272

Pepo 2 | Blog
Fun!

Insights

NI IPI PEPO YA ALLAH (SUBHANAHU WATAALA)

HITIMISHO

Wakati mmoja kulikaa watu watatu wakiwemo muislamu,mkristo na yahudi. Kila mmoja alikua akijisifia kua pepo ni yake na imeandaliwa kwa ajili yake. Mkirsto akajisifia kua Mtume wake Issa ni Ruhu-llah na kwamba atakuja duniani kueneza haki. Yahudi nae akajisifia kua amaeletewa mitume wengi waliokuwa watukufu kwahivyo pepo ni yake. Muislamu naye akajisifia kua mtume Muhammad(swalla Allahu alayhi wasallam) ndiye kipenzi cha Allah na ndio mtume wa mwisho hivyo pepo ni yake. 

Allah akateremsha aya isemayo: “(hiyo pepo) Si kwa matamanio yenu (waislamu) wala si kwa matamanio ya watu wa kitabu (mayahudi na manasara),atakaefanya uovu basi atalipwa….” Wanavyuoni wa Qur-an na baadhi ya masahaba akiwemo sayyidna Ally(radhi za Allah ziwe juu yao) wanasema hii ndio aya yenye kutisha zaidi ndani ya Qur-an,kwani yaonesha wazi iko tofauti na fikra za waislamu wa zama zetu. 

Tunadhani kua tukiwa na majina ya kina Muhammad na Ahmad na Khalid basi tutaingia peponi kisa ni waislamu,na hatutoadhibiwa kwa makosa yetu.Tutambue kua pepo haikuwekwa kwa kila anaejiita muislamu, lakini pepo imewekwa kwa walioamni kikweli, na wakafanya matendo mema.

Hakuna hata sehemu moja katika Qur-an iliyotaja kua kila atakaeitwa muislamu ataingia peponi tu bila ya kuadhibiwa kwa makosa yake kwanza, lakini sehemu zote Allah(subhanahu wataala) anasema wale watakaoamini na wakatenda yalo Mema. Amesema Allah(subhanahu wataala) katika Suratu Sabai 37 “Na si mali zenu wala watoto wenu watakaokukurubisheni kwetu katika daraja za (peponi) ila aliyeamini na akafanya matendo mema,basi hao watapata ujira mkubwa na wa ziada kwa yale waliyoyatenda..”. 

Kufanya matendo mema kunakusudiwa mengi,lakini kubwa lao ni kuepukana na kufuata matamanio ya nafsi, kwani pepo imezungushiwa yale yanayochukiwa na nafsi.

Muislamu anahitajika kufanya aliyoamrishwa na Allah, kuanzia nguzo za kiislamu na mengineo tunayotakiwa kuyafanya kama vile sadaka,kupigania dini ya Allah na mengine mengi kama alivyousiwa swahaba Muadh katika Hadithi ndefu ya Rasuul, na akahitimishiwa kwa kuwaambia, ili aweze kumiliki kufanya yote hayo ni lazima aweze kuumiliki ulimi wake, kwani ulimi na utupu ndio vitakavowakosesha watu pepo kulingana na Hadith Sahih ya Rasuul .

Hivyo basi milango ya pepo huachwa wazi ramadhan kwa kila anaetaka kuingia, na ya moto hufungwa.Tufanye juhudi ya kuipata pepo kwani Allah kila akimaliza kutaja neema za peponi husema ; "Kutokana na hayo washindane na wenye kushindana” na mahali pengine akasema ; "Kutokana na hayo(yani starehe za peponi) na wafanye wenye kufanya." Amesema Mtume wa Allah “Hakika bidhaa ya Allah ni ghali, hakika bidhaa ya Allah ni pepo." Basi na tuikimbilie hiyo bidhaa kabla hatujachelewa.

Allah atuwafikishe katika kheri na ataruzuku pepo na vyenye kutukurubisha kwenye pepo. Innahu waliyyu dhaalika wal-Qaadir alayhi.


photo credit: Theophilos via photopin cc

Comments

There are no comments

Post a comment