Insights
NI IPI PEPO YA ALLAH (SUBHANAHU WATAALA)
MAJINA YA PEPO
Pepo imetajwa kuwa na milango nane kama iliyvopokelewa katika hadithi mbalimbali. Hatahivyo, haikuja aya kuonesha milango ya pepo bali aya zimekuja kutaja majina ya pepo.
Miongoni mwa milango hiyo ya pepo, kuna mlango wa kulia utakaoingia wale watu sabini elfu bila ya hesabu wala adhabu, kuna mlango wa wafungaji unaoitwa Rayyan, kuna mlango wa wenye kukithirisha sala, kuna mlango wa wenye kukithirisha kutoa sadaka, kuna mlango maalum kwa mashahidi (waliokufa wakipigania dini ya Allah) na kuna mlango maalum kwa wenye kuzuia ghadhabu zao.
Hii milango imekuja katika Hadith mbalimbali za Rasuul (Swalla Allahu alayhi wasallam) na mengine miwili iliyobaki ni Qiyas ya wanavyuoni. Wallahu A’alam.
Ama majina ya pepo yaliyotajwa katika Qur-an ni:
1-Firdaus : Hii ni pepo ya daraja ya juu kwa na kwa lugha ya kimombo tutaiita “First Class." Sakafu yake ya juu ni Arshi Ya Allah, na mito yote peponi huanzia katika pepo hii. Waliyoandaliwa pepo hii wametajwa sifa zao mwanzo wa Suratul-Muuminuun aya ya 10-11 na ikamalizia kwa kusema “Hao ndio warithi (10) Ambao watarithi Firdaus milele (11)” Imepokelewa kuwa watakaoingia kupitia mlango wa kulia wa pepo basi makaazi yao ni katika pepo hii.
2-Jannaatu Adnin : Inasimuliwa kuwa pepo zote Allah aliziumba kwa kusema kua na zikawa, lakini pepo hii ameiumba kwa mikono yake. Ni pepo iliyotajwa mara nyingi katika Qur-an. Ama majina mengine ni: Jannaatul-khuld, Jannatul-Aaliyah, Jannaatu-Nnaim, Daarul-Akhirah, Daaru-Salaam, Daarul-Qaraar, Daarul-Mutaqin,na Daarul-Muqamah.
WAKE WA WATU WA PEPONI:
Tuanzie na wanawake wa jannah, kwani kama alivyotanguliza Allah kuwa kawapambia watu kupenda wanawake kama tulivyoona hapo kabla. Amesema Allah (subhanahu wataala) katika Suratul-Waaqiah aya ya 22-23. “(Watapewa humo) wanawake wenye macho mazuri na makubwa (22) (Wanapendeza) kama kwamba lulu zilofichwa (ndio kwanza zinapasuliwa)(23)”.
Wanawake wa jannah wamepewa jina la “Huurul-Ayn” kutokana na macho yao kuwa makubwa, ambayo yamekolea weusi wa mboni zao katika weupe wa macho yao.
Amesema Mtume swalla Allahu alayhi wassalam katika hadithi sahih ilopokewa na Bukhari na Muslim “…na kila mtu atakua na wake wawili,wanaoonekana uboko wa miguu yao,nyuma ya nyama zao,na hakutakua na mjane pepon." Akimaanisha kua ngozi zao zitaonesha mpaka kilicho ndani mfano wa kioo.
Vilevile Mtume amewasifu wanawake wa jannah kuwa lau kama mmoja wao ataletwa duniani basi harufu yake itaenea dunia nzima, na nuru yake itaangaza dunia nzima. (Hadith sahih Bukhari na Muslim).
Amesema Allah katika Suratu-Rahman aya ya 56-58 “Watakuwemo humo wanawake watulizao macho yao (56) Hawajaguswa na binaadamu yoyote wala jini kabla ya hapo (57) Kama kwamba ni yakuuti na marijani (58)” na Akasema tena katika Suratu-Swaffaat aya ya 48-49 “Pamoja nao watakua wanawake wenye macho mazuri na makubwa (48) Wanawake hao kama mayai yalohifadhiwa (49) " Amesema Mtume (swalla Allahu alayhi wasallam) ”….Hakika mmoja wenu atapewa nguvu za watu 100 katika kula,kunywa na kuingiliana na mkewe.” (Ahmad) Pamoja na uzuri wao lakini mwanamke mwema atakaeingia jannah atawazidi mahurul-ayn.
Usikose sehemu ya pili ya makala haya 'NI IPI PEPO YA ALLAH (SUBHANAHU WATAALA) nitazungumzia 'CHAKULA NA VINYWAJI VYA WATU WA PEPONI'
“NA KUMBUSHA, KWANI UKUMBUSHO HUWAFAA WAUMINI” (51:55).
photo credit: Giovanni 'jjjohn' Orlando via photopin cc

There are no comments