A PHP Error was encountered

Severity: Notice

Message: Only variable references should be returned by reference

Filename: core/Common.php

Line Number: 272

Mke wa Firaun | Blog
Fun!

Insights

Mke wa Firaun alijulikana kwa jina la Asia Bint Mzahim na aliishi wakati wa nabii Musa alyhi ssalaam. Ni mwanamke aliyejitolea kumlea nabii Musa aleyhi ssalaam baada ya kumuokota akielea mtoni. Asia na mumewe Firaun walikua hawajaaliwa mtoto.

Baada ya nabii Musa kukua na kwenda Madyan alikopewa utume na Allah (Subhanahu Wata‘ala), alirudi Misr kwa lengo la kuutangaza Uislamu, lakini hawakumuamini ila waliokuwa ni watu wa hali ya chini.

Miongoni mwa waliomuamini alikua ni huyu mama Asia aliyekuwa mke wa Firaun aliyemuasi Mola wake kupita maelezo mpaka kufikia kiwango cha kuwaambia watu wake kuwa yeye ndiye mungu wa juu kabisaa kama anavyotueleza Allah:

“Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi mkuu kabisa.” [an-Naziant 79: 24].

Na kama tunavyofahamu Firaun alikua ni miongoni mwa wafalme katika enzi hizo waliobarikiwa na kila walichohitaji katika starehe za kidunia, mama Asia pia alibarikiwa na haya yote. Lakini pamoja na hayo Allah alimruzuku imaan thabiti, mwanzo alificha imani yake lakini baadae aliamua kuidhihirisha na hapo ndipo Firaun alipoanza kumuadhibu adhabu kali huku akimlazimisha aachane na imani hiyo na kurudi kwenye kufru nako ni kuitakidi kuwa Firaun ndiye mungu.

Kwa kua Allah alimpa iman thabiti alibaki kwenye imani yake pamoja na adhabu hizo kali alizokuwa akiadhibiwa, na inasemekana karibu na kufa kwake alimuomba Allah ombi ambalo Allah analielezea ndani ya Quran kama ifuatavyo:

“Na Mwenyezi Mungu amewapigia mfano walio amini - mkewe Firauni, alipo sema ; Mola wangu Mlezi! Nijengee kwako nyumba Peponi, na uniokoe na Firauni na vitendo vyake, na uniokoe na watu madhaalimu.” [at-Tahrim 66:11].

Allah alimkubalia ombi na kumuandika miongoni mwa mwanawake wema na ndipo hata Mtume (Swalla Llahu Alyhi Wasallam) akamtaja kuwa ni miongoni mwa wanawake wanne waliokamilika.

Na inasemekana wakati yalipomjia mauti Allah alimuonesha nyumba yake aliyoiomba peponi hivyo alitabasamu na kucheka kwa furaha hali ya kuwa yumo kwenye adhabu kali anayopewa na Firaun (laanatullahi alayhi). Firaun alistaajabu na kuwaambia watu wake, "Naona umempata wendawazimu, kwani sisi tunamuadhibu na yeye anacheka."

Huyu ndiye mama Asia aliyekuwa mke wa Firaun aliyepata nyumba katika pepo ya Allah

photo credit: jj look via photopin cc

Comments

There are no comments

Post a comment