Insights
Mombasa ni mji mkongwe wa Afrika ya mashariki wenye sifa na tarekhe ndefu mno. Mji wenyewe ni kisiwa kilichozungukwa na maji pande zote ambacho kina mikondo miwili ya bahari. Mkondo wa kwanza ni wa kaskazini yaani maeneo ya bandari ya zamani ya Mombasa hadi Mwakirunge, maeneo haya yalikuwa makao ya Waswahili wa miji tisiya (Tisa twaifa) wakiwemo; Wamtwapa, wamvita, Wakatwa, Wabajuni ama Wagunya, Wakilifi,Wapaza,Wajomvu na Washaka. Kati ya makabila haya wengine walihamia Mombasa baada ya kuvundika( kuvunjika) kwa miji yao na wengine walikuja kwa khiari.
Kwenye mkondo wa bahari wa kusini wa kisiwa cha Mombasa waliishi waswahili wa miji mitatu (Thalatha twaifa) nao ni Wakilindini, Wachangamwe na Watangana ambao ndio wenyeji wa asili wa mji Mombasa. Maisha ya watu hao yalitegemeya sana uvuvi,ukulima na biashara. Kulingana na historia hapo kale palikuwa na uhusiano wa kibiashara baina ya miji ya pwani na Uarabuni,Uajemi, bara Hindi na Uchina. Siku hizo za kale biashara ilikuwa ni ya kubadilishana vitu. Kwa mfano Waarabu walileta tende,nguo, chumvi na vyenginevyo kutoka makwao hadi upwa huu wa Afrika mashariki. Baada ya kumaliza kukaa kwao nao walipeleka makwao vitu kama nazi, vyakula na mbao za kuundia majahazi.
Kuhusiana na jina la Mombasa historia yake ni ndefu, na kabla ya jina hilo la “Mombasa” kuna majina mengine sita yaliyolitangulia nayo ni; Faladi,Kongoweya,Gongwa, Mvita, Mji wa Kale, Nyali Kuu na hatimaye kuitwa Mombasa. Na yote haya ni mabadilifu kwa namna mbali mbali.
Kuna hoja tofauti zinazohusiana na usuli wa neno “Mombasa”. Hoja ya kwanza ni kuwa jina hili limetokana na maneno mawili ambayo ni “Mambo na Sasa”. Hoja ya pili ni kuwa limetokana na neno “Mwambadze?” (ambalo ni la Kimijikenda na maana yake ni kama wasemavyo waswahili wa kimvita- mwambaje?- yaani, kwa “Kiswahili sanifu” husemwa hamujambo?) Hoja nyengine ni kuwa jina hili limetokana na neno la Kiarabu “Nabasa” ambalo maana yake ni (mahali au mkao munapozungumzwa shughuli za kibiashara).
(Tazama, MEN AND MONUMENTS OF THE EAST AFRICAN COAST,LUTTERWORTH PRESS; LONDON UKURASA 118).
Nadharia nyengine ambayo ni ya wasemavyo wenyeji wa asili ya Mombasa ni kuwa jina hilo latokana na “Manpasa” hususan wazee hupaita Mambasa. Kuhusiana na usuli wa neno hilo kwa bahati mbaya sijafanikiwa kujua undani wake. Kuhusu usuli wa majina mengine ya mji huu mkongwe ni kama ifwatavyo; Kongoweya ni jina linalotokamana na neno la Kiswahili “Kongoni”- yaani karibuni na hini ni kwa ajili ya ukarimu wa wenyeji wa mji huu kwa kukaribisha wageni. Gongwa nalo ni neno la kingozi (Kiswahili cha kwanza) kwa maana ya ukuta. Kama ilivyokuwa katika miji ya pwani hapo kale yalizungukwa na kuta ndefu ambazo zilikuwa ni kinga dhidi ya mashambulizi kutoka kwa jamii zilokurubiana nazo. Kutokana na mapokezi ya mzee mmoja wa Mombasa (Ustadh Ahmad nassir Juma Bhalo) ni kuwa ukuta huo ulijengwa kwa ajili ya kuwazuwiya kabila moja iliyojulikana kwa jina la Warimba ambalo lilikuwa likila nyama za binadamu.
Jina lengine ni Mvita, na hili limetokana na hali ya mji ulipokuwa nyakati hizo.
Jina lenyewe latokamana na neno “vita” kwa kuwa mji wenyewe ulikuwa hauwishi vita- vita vya kupambana na wageni kama vile Wareno na Waarabu wa Oman waliokuja kuwatawala wenyeji, vita vya wenyewe kwa wenyewe na vita vya wenyeji wa Mvita na majirani zao (kwa mfano vita baina ya watu wa Mvita na watu wa Amu na vita baina ya Wapate na Wamvita). Inasemekana katika tarehe yake mji huu uliteketezwa moto zaidi ya mara tatu (Tizama; JUSTUS STRANDES, PORTUGUESE PERIOD IN EAST AFRICA, KENYA LITERATURE BUREAU 1960) Basi hali hiyo ya vita na moto mkali ndipo likazaliwa jina la Nyali Kuu, yaani miale mikubwa.
Baadhi ya majina haya yapatikana katika mashairi ya Yule Shaha wa Malenga wa zamanai wa Mombasa, Muyaka wa Muhaji aliyeishi baina ya mwaka wa 1776 na 1840 (Tizama; MOHAMED H ABDULAZIZ, MUYAKA:19TH CENTURY SWAHILI POPULAR POETRY, KENYA LITERATURE BUREAU 1979 ukurasa, 19).
Na katika shairi hilo Muyaka asema;
Kongowea ja mvumo, Mvita Mji wa Kale
Isokoma mititimo, na mayowe na kelele
Ni ya ngao na mafumo, na mata na panga kule
Wafileo walifile, mwoleza mfu nnani?
Gongwa ni mji muovu, viovu siukalile
Hupomosha wenye nguvu, wakawa kama wawele
Ikawatia kivumvu, nyoyo zikajaa tele
Wafileo walifile, mwoleza mfu nnani?
Gongwa la Mwana Mkisi*, Mvita mji wa ole
Ina waume watesi, kondo hawaiketele
Wenye ghamidha na kasi, na hasira za milele
Wafileo walifile, mwoleza mfu nnani?
Kwamba mujile na kondo, kuteta na simba wale
Vumiliani vishindo, vyao msivikimbile
Simba wanayo magando, makucha wayatanule
Wafileo walifile, mwoleza mfu nnani?
Ndiswi Nyali Kuu ndiswi, ndiswi msambe tufile
Ndiswi mwapigana naswi, naswi msitutawale
Ni swiswi nguli ni swiswi, tuvundao miji mile
Wafileo walifile, mwoleza mfu nnani?
Kivumbi cha Kongowea, kivumapo ni ja ndwele
Walo mbali husikia, kingurumo chenda kule
Watambaji hutambia, kwa mwendo wa pole pole
Wafileo walifile, mwoleza mfu nnani?
Ambayo maana yake kwa Kiingereza ni:
Kongowea (Mombasa) is like a roaring surf; Mvita is a city of old
It is always seething (with trouble), with so much noise and endless cries
It is a place full of shields, lances, bows and arrows, and long
swords
The dead are dead and gone! There is no feigning death (i.e. one
dies only once).
Gongwa (Mombasa) is a city full of malice (towards its enemy), so
bear no spite against it!
It thrusts down powerful ones and renders them as helpless as the sick
It shatters them and fills their hearts with sorrow
The dead...
Gongwa is the land of Mwana Mkisi*; Mvita, what an awesome
place it is!
It has warlike men who spoil for a fight
Men who are intransigent and obdurate, possessed of everlasting
fury
The dead....
If you (Omanis) have come seeking a war with our mighty lions
Then bear their clamorous wrath, and do not flee!
These lions have terrible claws that are already stretched out
The dead....
It is still we Mombasans, indeed it is. Do not think we are dead
It is us you are waging war against. We are fighting you so that
you may not rule over us
It is we demons who destroy yonder lands
The dead....
When Kongowea roars, it groans like someone suffering from a
terrible malady
Even those who are far away hear its rumblings
The warriors quietly take their positions and make their strategic
manoeuvres
The dead....
Mwana mkisi (Balqis) ni isimu ya aliyekuwa mtawala wa kale wa Mombasa, alikuwa mwanamke. Katika historia ya
Pwani ya Afrika ya Mashariki, kuna vipindi fulani ambapo utawala ulikua chini ya wanawake. Kwa mfano, Gongwa (Mombasa) kulikuwa na Mwana Mkisi (Balqis), Siu (kisiwa kilichoko kaskazini mwa
Pwani ya Kenya) kulikuwa na Mwana Musura, Unguja kulikuwa na
Mwana Aziza, Vumba kulikuwa na Mwana Shambi Shali, na kadhalika.
Kwenye mkondo wa bahari wa kusini wa kisiwa cha Mombasa waliishi waswahili wa miji mitatu (Thalatha twaifa) nao ni Wakilindini, Wachangamwe na Watangana ambao ndio wenyeji wa asili wa mji Mombasa. Maisha ya watu hao yalitegemeya sana uvuvi,ukulima na biashara. Kulingana na historia hapo kale palikuwa na uhusiano wa kibiashara baina ya miji ya pwani na Uarabuni,Uajemi, bara Hindi na Uchina. Siku hizo za kale biashara ilikuwa ni ya kubadilishana vitu. Kwa mfano Waarabu walileta tende,nguo, chumvi na vyenginevyo kutoka makwao hadi upwa huu wa Afrika mashariki. Baada ya kumaliza kukaa kwao nao walipeleka makwao vitu kama nazi, vyakula na mbao za kuundia majahazi.
Kuhusiana na jina la Mombasa historia yake ni ndefu, na kabla ya jina hilo la “Mombasa” kuna majina mengine sita yaliyolitangulia nayo ni; Faladi,Kongoweya,Gongwa, Mvita, Mji wa Kale, Nyali Kuu na hatimaye kuitwa Mombasa. Na yote haya ni mabadilifu kwa namna mbali mbali.
Kuna hoja tofauti zinazohusiana na usuli wa neno “Mombasa”. Hoja ya kwanza ni kuwa jina hili limetokana na maneno mawili ambayo ni “Mambo na Sasa”. Hoja ya pili ni kuwa limetokana na neno “Mwambadze?” (ambalo ni la Kimijikenda na maana yake ni kama wasemavyo waswahili wa kimvita- mwambaje?- yaani, kwa “Kiswahili sanifu” husemwa hamujambo?) Hoja nyengine ni kuwa jina hili limetokana na neno la Kiarabu “Nabasa” ambalo maana yake ni (mahali au mkao munapozungumzwa shughuli za kibiashara).
(Tazama, MEN AND MONUMENTS OF THE EAST AFRICAN COAST,LUTTERWORTH PRESS; LONDON UKURASA 118).
Nadharia nyengine ambayo ni ya wasemavyo wenyeji wa asili ya Mombasa ni kuwa jina hilo latokana na “Manpasa” hususan wazee hupaita Mambasa. Kuhusiana na usuli wa neno hilo kwa bahati mbaya sijafanikiwa kujua undani wake. Kuhusu usuli wa majina mengine ya mji huu mkongwe ni kama ifwatavyo; Kongoweya ni jina linalotokamana na neno la Kiswahili “Kongoni”- yaani karibuni na hini ni kwa ajili ya ukarimu wa wenyeji wa mji huu kwa kukaribisha wageni. Gongwa nalo ni neno la kingozi (Kiswahili cha kwanza) kwa maana ya ukuta. Kama ilivyokuwa katika miji ya pwani hapo kale yalizungukwa na kuta ndefu ambazo zilikuwa ni kinga dhidi ya mashambulizi kutoka kwa jamii zilokurubiana nazo. Kutokana na mapokezi ya mzee mmoja wa Mombasa (Ustadh Ahmad nassir Juma Bhalo) ni kuwa ukuta huo ulijengwa kwa ajili ya kuwazuwiya kabila moja iliyojulikana kwa jina la Warimba ambalo lilikuwa likila nyama za binadamu.
Jina lengine ni Mvita, na hili limetokana na hali ya mji ulipokuwa nyakati hizo.

Baadhi ya majina haya yapatikana katika mashairi ya Yule Shaha wa Malenga wa zamanai wa Mombasa, Muyaka wa Muhaji aliyeishi baina ya mwaka wa 1776 na 1840 (Tizama; MOHAMED H ABDULAZIZ, MUYAKA:19TH CENTURY SWAHILI POPULAR POETRY, KENYA LITERATURE BUREAU 1979 ukurasa, 19).
Na katika shairi hilo Muyaka asema;
Kongowea ja mvumo, Mvita Mji wa Kale
Isokoma mititimo, na mayowe na kelele
Ni ya ngao na mafumo, na mata na panga kule
Wafileo walifile, mwoleza mfu nnani?
Gongwa ni mji muovu, viovu siukalile
Hupomosha wenye nguvu, wakawa kama wawele
Ikawatia kivumvu, nyoyo zikajaa tele
Wafileo walifile, mwoleza mfu nnani?
Gongwa la Mwana Mkisi*, Mvita mji wa ole
Ina waume watesi, kondo hawaiketele
Wenye ghamidha na kasi, na hasira za milele
Wafileo walifile, mwoleza mfu nnani?
Kwamba mujile na kondo, kuteta na simba wale
Vumiliani vishindo, vyao msivikimbile
Simba wanayo magando, makucha wayatanule
Wafileo walifile, mwoleza mfu nnani?
Ndiswi Nyali Kuu ndiswi, ndiswi msambe tufile
Ndiswi mwapigana naswi, naswi msitutawale
Ni swiswi nguli ni swiswi, tuvundao miji mile
Wafileo walifile, mwoleza mfu nnani?
Kivumbi cha Kongowea, kivumapo ni ja ndwele
Walo mbali husikia, kingurumo chenda kule
Watambaji hutambia, kwa mwendo wa pole pole
Wafileo walifile, mwoleza mfu nnani?
Ambayo maana yake kwa Kiingereza ni:
Kongowea (Mombasa) is like a roaring surf; Mvita is a city of old
It is always seething (with trouble), with so much noise and endless cries
It is a place full of shields, lances, bows and arrows, and long
swords
The dead are dead and gone! There is no feigning death (i.e. one
dies only once).
Gongwa (Mombasa) is a city full of malice (towards its enemy), so
bear no spite against it!
It thrusts down powerful ones and renders them as helpless as the sick
It shatters them and fills their hearts with sorrow
The dead...
Gongwa is the land of Mwana Mkisi*; Mvita, what an awesome
place it is!
It has warlike men who spoil for a fight
Men who are intransigent and obdurate, possessed of everlasting
fury
The dead....
If you (Omanis) have come seeking a war with our mighty lions
Then bear their clamorous wrath, and do not flee!
These lions have terrible claws that are already stretched out
The dead....
It is still we Mombasans, indeed it is. Do not think we are dead
It is us you are waging war against. We are fighting you so that
you may not rule over us
It is we demons who destroy yonder lands
The dead....
When Kongowea roars, it groans like someone suffering from a
terrible malady
Even those who are far away hear its rumblings
The warriors quietly take their positions and make their strategic
manoeuvres
The dead....
Mwana mkisi (Balqis) ni isimu ya aliyekuwa mtawala wa kale wa Mombasa, alikuwa mwanamke. Katika historia ya
Pwani ya Afrika ya Mashariki, kuna vipindi fulani ambapo utawala ulikua chini ya wanawake. Kwa mfano, Gongwa (Mombasa) kulikuwa na Mwana Mkisi (Balqis), Siu (kisiwa kilichoko kaskazini mwa
Pwani ya Kenya) kulikuwa na Mwana Musura, Unguja kulikuwa na
Mwana Aziza, Vumba kulikuwa na Mwana Shambi Shali, na kadhalika.
October 13, 2015
Woow this is awsome.am originally born and raised in mombasa;and all my age never knew about this.please guide me for more books if any where I can learn more.Thanks in advance.