A PHP Error was encountered

Severity: Notice

Message: Only variable references should be returned by reference

Filename: core/Common.php

Line Number: 272

Umoja ni Nguvu | Blog
Fun!

Insights

Mombasa Toa Donge Lako ni kikundi kiluchobuniwa katika mtandao wa kijamii wa facebook takriban mwaka mmoja na nusu uliopita miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu wa 2013. Wakati huo lengo kuu likiwa ni kuwapa watu wa Mombasa jukwaa la kuwasilisha minukuniko yao ya kisiasa pamoja na kubadilishana mawazo yatakayosaidia kuboresha uongozi wa Mombasa.

Kama ilivyoada siasa huja na kuenda lakini wanajamii hubakia palepale. Hivyo basi baada ya uchaguzi wa mwaka 2013 kulikuwepo na haja ya kubakisha kundi hili ambalo lilisalijiliwa kama shirika la kijamii na kuitwa Donge La Mombasa Welfare Group. Wakati huu lengo likiwa ni kuboresha maisha ya wanati (wenyeji) wa Mombasa kupitia umoja na kujitolea. Hii imethibitishwa kwenye nembo ya kundi hili inayosema "Rebuilding our community through unity and sacrifice."

DLMWG imefanikiwa kuunganisha wenyeji wa Mombasa wanaoishi katika sehemu mbali mbali za ulimwengu. Umoja na upendo unaoshuhudiwa katika shirika hili umevutia hadi watu wasio wenyeii wa Mombasa. Watu hawa pia wamekuwa nguzo muhimu katika shirika hili. Vilevile, kutokana na mafanikio ya kundi hili, kumechipuka makundi mengi yanayofuata mfano mwema wa Donge. Yani DLMWG imekuwa kielelezo chema kwa jamii. Cha kutia moyo zaidi ni kuwa wanachama wa kundi hili wanafanya kazi kwa kujitolea. Hakuna hata mwanachama mmoja anayelipwa kwani shirika hili sio la kibiashara.
 
IMG-20140424-WA0000
Jamila Al Jabry, mueka hazina wa donge akiwa na Khadija aliyekatwa mguu baada ya kuuguwa saratani ya mfupa

Tangu kubuniwa kwake, wanachama wa kundi hili chini ya uongozi wa bodi yake wamefanikiwa kutekeleza miradi kadha wa kadha iliyosaidia watu wasiojiweza kwenye jamii. Fedha zinazotumika kutekeleza miradi ya kuendeleza jamii hutoka mifukoni mwa wasamaria wema. Nitadokeza tu baadhi ya juhudi zake zilizowaleta watu pamoja na kusaidia palipohitajika. 

Donge imefanikiwa kukusanya vyakula, nguo, vitabu, sabuni miongoni mwa bidhaa nyingine na kuzipeleka kwa makaazi ya mayatima katika sehemu tofauti za eneo la pwani. Donge imefanikiwa kukusanya fedha na kufadhili watoto wawili wagonjwa kupata matibabu. Khadija (14yrs) akiwa na saratani ya mguu na Fatma (Mungu amrehemu) aliyekuwa na ugonjwa wa moyo aliyefariki alipokua nchini India kwa matibabu. Vilevile Donge ilisimamia ujenzi wa matanki mawili ya maji (kila moja likiwa na uwezo wa kubeba lita 10, 000 za maji) katika kisiwa cha Wasini kilicho eneo la Pwani Kusini. Kiufupi nikiendelea kuelezea kuhusiana na mazuri ya umoja wa jamaa hawa wa Donge, sitomaliza sasa.

Kundi hili limedhihirisha wazi kuwa watu wakishikana kwa udugu na upendo hakuna lisilowezekana. Ukitaka kujua mengi kuhusiana na kundi hili tembelea tovuti www.dongelamombasa.com ama pia tembelea ukurasa katika mtandao wa facebook kwa jina Mombasa Toa Donge Lako.
 
IMG_20140511_140129
Wanadonge wakiwa nje ya hifadhi ya maji waliyojenga Wasini


Comments

There are no comments

Post a comment