A PHP Error was encountered

Severity: Notice

Message: Only variable references should be returned by reference

Filename: core/Common.php

Line Number: 272

MADHARA YA MAO, TAMBU NA TUMBAKU (UGORO) - | Blog
Fun!

Insights

TAHADHARI – Picha za taarifa hii huenda zikakukirihisha.      

“Jina langu ni Hassan Ali. Nina miaka 70. Maisha yangu yote nimekuwa mraibu wa tambu na mao. Sasa najuta sana kutumia uraibu huo. Hivi sasa niko kitandani hospitali ya Pandya mjini Mombasa nikiwa mgonjwa wa saratani ya mdomo (mouth cancer) iliyosababishwa na uraibu huo. Siwezi kula, siwezi kunywa, siwezi kucheka, siwezi kusema. Chakula kikubwa nipewacho ni maji tena nanyishwa vitone vitone kwa sindano kama mtoto wa ndege. Madaktari wameshindwa kunitibu. Nimekwenda mpaka India nikaambiwa nirudi kwetu Mombasa na nisubiri siku yangu ya kukutana na Maulana. Sina dawa ila ni kungoja siku yangu ifike. Leo mjukuu wangu Ahmed Juma Bhalo alikuja na wenzake kunitembelea na kunichangia damu. Nawashukuru sana. Sasa basi mimi kama babu yenu nachukuwa fursa hii kuwaomba muwachane na uraibu wa aina yoyote. WALLAHY hakuna uraibu mzuri. Nimempa Ahmed ruhusa ya kunipiga picha na kuwaonesha nyinyi wajukuu zangu ndio mushuhudie nisemacho. Na mukitaka njooni munione hospitalini. Mwenyewe niko radhi na nitafurahi mukija kunitembelea. Naomba dua zenu kwa wingi. Shukran sana.” END.10408561_272266899613016_4752840294635839686_n      

photo credit: Curtis Gregory Perry via photopin cc

Comments

There are no comments

Post a comment