A PHP Error was encountered

Severity: Notice

Message: Only variable references should be returned by reference

Filename: core/Common.php

Line Number: 272

Mchimba Riziki | Blog
Fun!

Life Style

(AN INSPIRING BROTHER ) -MCHIMBA RIZIKI - Omar Mwenye Bashee maarufu Omar Nyonda alizaliwa mwaka 1982 katika kaunti ya Malindi kwenye familia ya watoto watatu. Alibahatika kupata elimu ya madrassa pamoja na ya shule lakini kutokana na hali ngumu ya maisha alilazimika kukatiza kiu yake ya masomo akiwa darasa la tatu, umri wa miaka 9, kwenye shule ya msingi ya Sir Ali.

Kukatizwa kwa masomo yake hakukuwa mwisho wa maisha yake, Nyonda alijuwa fika maisha mbele yake ni magumu na ni lazima kujikaza kibwewe na kupambana katika kusukuma gurudumu la maisha.

Alipokua na umri wa miaka 12 alibahatika kupata kibarua chake cha kwanza. Amini usiamini licha ya umri wake mdogo aliingilia kazi ya uhamali (kubeba mizigo). Kazi yake hii ilijumuisha kubeba magunia ya unga pamoja na keni za mafuta. Nyonda aliifanya kazi hii ngumu bila familia yake kujuwa.
"Kuna jamaa yangu aliniona sokoni napambana na magunia akenda kumwambia mama. Mamangu hakufurahia kazi hii na akaniomba niwachane nayo.Kazi yenyewe ilikua nalipwa shilingi mia kwa siku ama nyakati zengine silipwi kamwe na narudi nyumbani mikono mitupu," Nyonda alinambia.

Kwa kuwa hakutaka kumuudhi mamake mzazi kijana huyu jasiri aliwacha kazi hiyo na kuamua kufungua biashara yake binafsi. "Niliweka kijimeza kidogo sokoni huko Malindi nikawa nauza betri za saa na za redio. Leo napata, kesho nakosa." Wakati wa kazi yake hii kijana huyu wa kipekee katika familia iliyokua na pandashuka nyingi, alipata ujuzi na kukuza biashara yake. "Niliona ntauza betri mpaka lini? Nikaamua kuingilia ufundi wa redio pamoja na kuuza redio."
1796556_10202411096112171_1193130289_n
Omar Nyonda aliamini kuwa atafutae hachoki na akichoka basi ujuwe ameshapata. Wakati mmoja mjini Malindi baraza la kaunti hiyo liliamua kuwafurusha wachuuzi (hawkers) wote babarani na kuvunja vibanda vyao. Maadamu alikua kijana mchapa kazi mwaka 2007 alifunga safari na kuja mjini Mombasa kutafuta riziki yake ya halali. "Hapa Mombasa nilifunguwa biashara ya kuuza tv, redio pamoja na kuzitengeneza mwaka 2007 wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi."

Nyonda anajivunia sana kazi yake. "Alhamdulilahi sasa nimeweza kukodisha duka, kuajiri mtu na kuwasaidia wazazi wangu pamoja na dada zangu wanapokuwa na shida."

Je ana ushauri gani kwa vijana? "Maisha ya siku hizi ni kung'ang'ana. Ukilala basi maisha yatakulalia."

Kama ajira yoyote ile kazi anayoifanya jamaa huyu ina changamoto zake. "Kweli napitia mazito ya hapa na pale lakini wajua mgaa gaa na upwa hali wali mkavu. Pia kinachonitia moyo zaidi wa kupambana na kazi hii ni wazazi wangu kwani mimi ndiye kijana wa pekee katika familia."

Je ana ndoto gani maishani mwake? "Mungu akinipa uwezo nataka kupanua biashara yangu. Pia nna hamu kubwa sana ya kutaka kusomea lugha ya kizungu lakini uwezo ndio sina."

Je ashaoa? " Bado sijapata kheri yangu."

Huku vijana wengi nchini Kenya wakilalamimikia ukosefu wa ajira, bidii ya Nyonda ni funzo kamili kuwa mustakabali wa maisha yetu upo mikononi mwetu...END

WASILIANA NA OMAR NYONDA IWAPO UNAHITAJI FUNDI WA TV AMA REDIO KWENYE NAMBARI - 0721939453. VILEVILE UNAWEZA KUWASILIANA NAE IWAPO UNA UWEZO WA KUMSADIA KUSOMEA LUGHA YA KIZUNGU.

SHUKRAN.

Comments

There are no comments

Posting comments after has been disabled.