A PHP Error was encountered

Severity: Notice

Message: Only variable references should be returned by reference

Filename: core/Common.php

Line Number: 272

Safari Hatari | Blog
Fun!

Current Affairs

Siku moja baada ya ajali mbaya ya barabarani iliyohusisha basi la kampuni ya Najaah (Lamu - Mombasa) kutokea eneo la Marereni na kupelekea vifo vya watu watano, nilibahatika kuabiri basi kutoka Lamu na kuelekea mjini Mombasa.1521929_246602712166339_1613488267_n

 

Wakati wa safari yangu nilishuhudia mambo ya kuogopesha, mambo yanayohatarisha maisha ya abiria. Basi nililoabiri lilibeba abiria kupita idadi inayotakikana. Ukitazama kwa umakini picha hizi utaona baadhi ya abiria (wakiwemo watoto) wameketi katikati ya njia juu ya kreti za soda. Huku wengine wakiwa wamesimama kwa kukosa sehemu ya kuketia.

 

Barabarani tulikumbana na vizuizi vya polisi, hatahivyo hakuna hata polisi mmoja aliyedadisi idadi ya abiria iliyopita kiasi. Je, sehemu hii ya Kenya magari ya uchukuzi wa umma yanaruhusiwa kubeba abiria kupita idadi inayostahili?

[caption id="attachment_787" align="aligncenter" width="300"]Barabarani tulikumbana na vizuizi vya polisi, hatahivyo hakuna hata polisi mmoja aliyedadisi idadi ya abiria iliyopita kiasi. Barabarani tulikumbana na vizuizi vya polisi, hatahivyo hakuna hata polisi mmoja aliyedadisi idadi ya abiria iliyopita kiasi.[/caption]

Kando na hilo, basi nililopanda sidhani kama linapaswa kuwa barabarani kwani safari nzima linayumbayumba. Isitoshe basi lenyewe halina hata mikanda ya usalama. Je, tuombe John Michuki arudishwe duniani ndio idara ya uchukuzi iboreke?

 

 

Yote tisa la kumi serikali inafaa kuwajibika katika kulinda maisha ya Wakenya na kukomesha ulafi wa wafanyibiashara kwenye sekta ya uchukuzi. Vilevile serikali inapaswa kuchangamka na kukarabati barabara inayounganisha Garseni na Lamu, kwani hali yake inahatarisha maisha ya wasafiri. Miaka nenda miaka rudi barabara hii imekuwa haitamaniki.

Comments

There are no comments

Posting comments after has been disabled.